-
Fadavi: Wamarekani wamekimbia umbali wa zaidi ya Kilomita 1,000 kutoka Iran
Oct 06, 2026 04:16Aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya KIislamu (SEPAH) ambaye hivi sasa ni mkuu wa timu ya washauri wa Kamanda Mkuu wa jeshi hilo amesema: "Wamarekani wamekimbia umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 kutoka kwenye mipaka ya Iran; na hatua hiyo haikutokana na hiari yao wenyewe, bali ni kutokana na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
-
Kamanda Mkuu atoa onyo kali: Moto wa vita vyovyote vipya dhidi ya Iran, utamwakia kila mtu
Oct 05, 2026 11:39Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Ali Abdollahi, ameonya kuwa vita vyovyote vipya vitakavyoanzishwa dhidi ya Iran vitakuwa na madhara makubwa kwa pande zote na "moto wake utamwakia kila mtu".
-
Iran yatwaa taji la dunia la Olimpiadi ya Astronomia na Astrofizikia kwa mara ya 3 mfululizo
Oct 05, 2026 10:51Wanafunzi wa Iran wamenyakua medali tano za dhahabu katika Olimpiadi ya Kimataifa ya Astronomia na Astrofizikia iliyofanyika nchini Vietnam, na kutwaa ubingwa wa dunia wa mashindano hayo ya kielimu kwa mwaka wa tatu mfululizo.
-
Msimamo Rasmi wa Iran Kuhusu Safari ya Netanyahu huko Abu Dhabi; Onyo kwa UAE na Eneo Zima
Oct 05, 2026 07:40Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitoa taarifa rasmi tarehe 29 Septemba 2026, ikijibu ziara ya siri ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, huko Abu Dhabi na mkutano wake na Sheikh Mohamed bin Zayed, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
-
Kwa nini UAE imekariri tena madai yake kuhusu visiwa vitatu vya Iran?
Oct 05, 2026 06:25Katika kujibu madai ya mara kwa mara ya UAE kuhusu visiwa vitatu vya Iran, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza tena msimamo wa Tehran, akisema kuwa Abu Musa, Tunb Kubwa na Tunb Ndogo ni sehemu isiyotenganishika ya ardhi ya Iran na kwamba kuraririwa kwa madai yasiyo na msingi hakubadilishi chochote kuhusu uhalisia wa kihistoria na kisheria wa visiwa hivyo.
-
Spika Qalibaf: Ikiwa masharti saba ya Iran hayatatekelezwa, Mlango wa Hormuz hautafunguliwa
Oct 05, 2026 03:56Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa Iran haitaufungua Mlango wa Hormuz hadi masharti saba yaliyowekwa na Tehran, kwa mujibu wa makubaliano ya Islamabad, yatakapotekelezwa.
-
Iran yawaonya washirika wa US katika eneo: Kutumiwa tena ardhi zenu kutakabiliwa na jibu 'tofauti'
Oct 05, 2026 03:46Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, ameonya kwamba utumiwaji wowote wa ardhi za nchi za eneo hili utakaofanywa katika siku za usoni kwa ajili ya kuishambulia Jamhuri ya Kiislamu utasababisha jibu tofauti na kali, na kusisitiza kwamba Tehran inatarajia majirani zake watazingatia kanuni ya ujirani mwema.
-
Iran: Makombora yetu mapya yana kasi zaidi na yanapiga mbali zaidi
Oct 04, 2026 11:08Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia upeo na kasi ya makombora mapya ya Iran na kusisitiza kuwa, makombora yetu mapya yanapiga umbali mkubwa zaidi na kwa kasi kubwa zaidi.
-
Iran: Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hayapaswi kuweko Marekani
Oct 04, 2026 11:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa: Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hayapaswi kuweko nchini Marekani kwani nchi hiyo si mwenyeji mzuri hata kidogo wa chombo hicho kikubwa zaidi cha kimataifa duniani.
-
Chombo kipya cha Iran kurushwa anga za juu karibuni hivi
Oct 04, 2026 10:53Mjumbe mmoja wa Taasisi ya Utafiti wa Anga za Juu (Astronautics Research Institute) iliyoko chini ya Taasisi ya Utafiti wa Anga (Aerospace Research Institute) ya Wizara ya Sayansi ya Iran ametangaza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu karibuni hivi itazindua chombo kipya cha anga za mbali.