Pars Today
Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran, amesema kwamba Shahidi Hassan Nasrullah alikuwa shakhsia mwenye kutafakari na kuchambua mambo ipasavyo na kuongeza kuwa: Shahidi huyu wa daraja ya juu alikuwa ni mchanganyiko adimu wa uwezo wa fikra na kutenda."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekutana na Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi wa Sudan, Gibril Ibrahim Mohamed, aliyeko safarini mjini Tehran kujadili uhusiano wa pande mbili, biashara na uchumi.
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Ghalibaf amesema kuuawa shahidi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah kulifichua namna utawala wa Kizayuni usivyoheshimu mapatano ya aina yoyote.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, madai kwamba Iran ilihusika katika jaribio la kuwaua viongozi wa zamani au wa sasa wa Marekani yanakanushwa vikali na hayana msingi wowote.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kisasi cha hivi karibuni cha Iran dhidi ya Israel kilionyesha sehemu ndogo tu ya uwezo wa taifa hili.
Rais wa Ukraine amesema, madai hewa yaliyotolewa na nchi za Ulaya dhidi ya Iran kwamba imeipelekea Russia makombora ya balestiki hayana ukweli.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa kiongozi wa muqawama (mapambano ya Kiislamu), mwanazuoni wa mujahidina na kamanda shupavu, shujaa na mbunifu ambaye aliigeuza harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ngome imara.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali kitendo cha hivi karibuni cha utawala ghasibu wa Israel cha uchokozi dhidi ya vituo kadhaa vya Iran, na kukitaja kuwa ni ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya kujtawala ya Iran.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Haijalishi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nani ameshinda uchaguzi wa rais nchini Marekani.
Waziri wa Uchumi na Fedha wa Iran na Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi wa Sudan wamekutana na kujadili upanuzi wa uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.