-
Eslami: Vitisho vya maadui vinaendelea; hali ya kuaminiana na IAEA inapasa kujengwa upya
Sep 18, 2025 07:24Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema vitisho kutoka kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu vinaendelea tangu kujiri mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii.
-
Iran yayataja kuwa ya kipuuzi madai ya Marekani kuhusu mpango wake wa makombora
Sep 18, 2025 04:40Iran imetaja kuwa ya kipuuzi madai ya Marekani kuhusu ustawi wake katika sekta ya makombora, ikielezea mpango huo kuwa wa kujihami dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel.
-
Jenerali: Uwezo wa Iran wa kivita unawazuia maadui kuanzisha mashambulizi mapya
Sep 18, 2025 06:05Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, amepongeza kuimarika kwa uwezo wa kujihami wa taifa , akisisitiza kuwa utayari wa Iran wa kivita umezuia maadui kuanzisha duru mpya ya mashambulizi dhidi ya nchi.
-
Kiongozi wa Mapinduzi aipongeza timu ya miereka kwa kutwaa ubingwa wa dunia
Sep 17, 2025 13:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mchezo wa miereka ya freestyle kwa kutwaa taji la ubingwa wa dunia katika Mashindano ya Miereka ya Dunia ya 2025 yaliyofanyika mjini Zagreb, Croatia.
-
Iran yatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya jasusi wa Mossad ya Israel katika Vita ya Siku 12
Sep 17, 2025 12:25Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Babak Shahbazi, raia aliyekutwa na hatia ya kushirikiana na shirika la kijasusi la utawala wa Israel, Mossad, kwa kutoa taarifa nyeti kuhusu maeneo ya kiusalama ya Iran wakati wa vita ya siku 12 vya kichokozi vya utawala huo mwezi Juni.
-
Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Iran akutana na Bin Salman mjini Riyadh
Sep 17, 2025 06:47Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Ali Larijani amekutana na Mwanamfalme wa Saudiam Mohammed bin Salman mjini Riyadh kujadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya kieneo.
-
Iran yalaani uingiliaji wa Marekani katika masuala yasiyoihusu
Sep 17, 2025 06:47Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa kauli kali ya kulaani unafiki, hadaa na uadui wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa kisingizio cha kumbukumbu ya machafuko ya Shahrivar mwaka 1401 Hijria Shambia na kusema kuwa huo mfano wa wazi wa uingiliaji wa masuala ya Iran ambayo hayaihusu Marekani ndewe wala sikio.
-
Bahreini: Uvamizi wa Israel dhidi ya Qatar, tishio kwa usalama wa eneo na kimataifa
Sep 17, 2025 02:43Balozi wa Iran katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi amelaani vikali uvamizi wa karibuni wa utawala wa Israel dhidi ya Qatar na kuitolea wito jamii ya kimataifa kuchukua hatua kuzuia kuendelea vitendo kama hivyo ambavyo vinatishia kila mtu katika kanda hii.
-
Rais Pezeshkian: Saudi Arabia inabeba 'jukumu zito' kwa umoja wa Waislamu dhidi ya Israel
Sep 16, 2025 12:12Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa mataifa makubwa ya Kiislamu, hasa Saudi Arabia yanabeba "jukumu zito sana" katika hali ya sasa, na kwamba kuwepo umoja kati ya nchi za Kiislamu kutazuia uchokozi wa Israel.
-
Baqaei: Rasimu ya azimio inasisitiza kuzuiwa mashambulizi dhidi ya taasisi za nyuklia za malengo ya kiraia
Sep 16, 2025 12:11Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametoa taarifa kuhusu rasimu ya azimio la Iran katika Mkutano Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unaoendelea Vienna, Austria ambayo inalenga kuzuia mashambulizi kwenye vituo vya nyuklia vinavyoendesha shughuli zake kwa malengo ya amani na ya kiraia.