-
SEPAH: Iran itapiga meli za Marekani Bahari ya Hindi iwapo kutatokea vita vipya
Sep 28, 2026 03:34Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ameonya kuwa, Iran itapiga meli za Marekani katika Bahari ya Hindi iwapo Washington itaanzisha vita vipya vya uchokozi dhidi ya Tehran.
-
Rais Pezeshkian: Trump anaota ndoto za kuiangamiza Iran
Sep 27, 2026 13:00Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, “Rais wa Marekani anaota ndoto za kuifuta, kuiangamiza na kuipindua Iran, kwa sababu taifa letu linafanya juhudi kwa nguvu na uthabiti, na litaweza kushinda vikwazo vyote.”
-
Meja Jenerali Hatami: Ikiwa Iran haitafanya biashara, basi hakuna mtu yeyote atakayeweza kufanya biashara
Sep 27, 2026 12:58Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaonya maadui kwamba: “Iwapo Iran haitaweza kufanya biashara, na iwapo Iran haitaweza kuishi, basi hakuna mtu atakayeweza kufanya biashara wala kuishi.”
-
Araghchi: Ukosefu wa usalama katika Lango Bahari la Hormuz ni matokeo ya uvamizi wa Marekani na Israel
Sep 27, 2026 03:30Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, ukosefu wa usalama katika Mlango Bahari wa Hormuz na kuvurugika usafiri wa majini ni matokeo ya moja kwa moja ya hatua za uchokozi na uvamizi uliofanywa na Marekani na utawala ghasibu wa Israel.
-
Iran yatengeneza chanjo za wanyama wa majini kwa kutegemea teknolojia ya ndani
Sep 27, 2026 02:59Watafiti wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu ya Tehran wamefanikiwa kupata ujuzi wa kiteknolojia wa kutengeneza chanjo za wanyama wa majini.
-
Wizara ya Ulinzi: Miundombinu ya ulinzi ya Iran ya chini ya ardhi inavuruga mahesabu ya adui
Sep 26, 2026 11:25Msemaji wa Wizara ya Ulinzi, Brigedia Jenerali Reza Talaei-Nik, amesema, katika miaka ya hivi karibuni, Iran imesambaza sehemu ya uwezo wa kimkakati wa vikosi vyake vya ulinzi katika maeneo salama na miundombinu ya chini ya ardhi, hatua ambayo imekanganya na kuvuruga mahesabu ya adui."Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu ya uwezo wa kimkakati wa vikosi vya ulinzi imewekwa katika maeneo salama na miundombinu ya chini ya ardhi; hatua hii imevuruga mahesabu ya adui kuhusiana na uwezo wa ulinzi wa
-
Uchambuzi wa hotuba ya Pezeshkian katika Umoja wa Mataifa: Muqawama imara na diplomasia yenye masharti
Sep 26, 2026 08:00Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambayo iligusia masuala muhimu kimataifa imewavutia wengi ulimwenguni na hasa vyombo vya habari.
-
Kwa nini fikra ya "Ulinzi" inasalia kuwa takatifu kwa Wairani?
Sep 26, 2026 06:25Kwa Waajemi au Wairani, "Ulinzi Mtakatifu" si simulizi ya vita pekee, bali ni fikra iliyokita mizizi katika utambulisho na utamaduni, ikithibisha uzoefu wa mapambano, kujitegemea, umoja wa kitaifa na muqawama dhidi ya vitisho vya nje.
-
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa: Jukwaa la Iran Kudai Haki
Sep 26, 2026 05:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Mwaka huu, Umoja wa Mataifa utatumika kama jukwaa la kuelezea masaibu yanayowakabili wananchi wa Iran, mashahidi wa shule ya Minab na Kiongozi Mkuu aliyeuawa shahidi."
-
EU lazima iwajibishwe kwa uvamizi wa Marekani nchini Iran
Sep 26, 2026 03:28Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Ulaya na wanachama wa NATO lazima wawajibishwe kwa uvamizi wa Marekani dhidi ya Iran.