-
Iran: Azimio la Marekani lililopasishwa na UN kuhusu Gaza linahalalisha ukaliaji mabavu
Nov 19, 2025 12:46Iran imekosoa azimio lililoandaliwa na Marekani na kupasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloweka utaratibu wa kutumwa Gaza usimamizi wa nchi ajinabi na kutahadharisha kuwa azimio hilo linadhoofisha haki za msingi za watu wa Palestina.
-
Grossi: Wakaguzi wa wakala wa IAEA wamerejea Iran
Nov 19, 2025 12:05Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema katika kikao cha robo mwaka cha Bodi ya Magavana ya wakala huo kwamba: "Wakaguzi wa IAEA wamerejea Iran na wamefanya ukaguzi katika vituo ambavyo havikuathiriwa na mashambulizi ya Juni, lakini ushirikishwaji zaidi unahitajika ili kurejesha ukaguzi kamili."
-
Rais Pezeshkian: Iran inalenga kuimarisha uhusiano na Oman
Nov 19, 2025 06:59Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu uhusiano imara kati ya Iran na Oman, na kueleza kuwa Tehran ina imani kwamba uhusiano wa pande mbili utaendelea kukua kwa "nguvu na uthabiti.
-
Bin Salman: Tunajaribu kupatanisha baina ya Iran na Marekani
Nov 19, 2025 02:49Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye kimsingi ndiye kiongozi nambari moja wa nchi hiyo amesema: "Tutafanya kila tunavyoweza kuhakikisha kunafikiwa makubaliano kati ya Iran na Marekani; (ninaamini kwamba) Tehran pia iko tayari kusaini makubaliano hayo."
-
Iran yapendekeza mfumo wa malipo wa kidijitali katika Jumuiya ya Shanghai
Nov 19, 2025 02:24Mohammad Reza Aref Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran amependekeza kuanzisha mfumo wa pamoja wa malipo ya kidijitali ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi 10 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
-
Vipi mauzo ya Iran kwa Afrika yamevunja rekodi katika nusu ya kwanza ya mwaka 1404 Hijria Shamsia?
Nov 18, 2025 12:07Mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika yaliongezeka maradufu katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu (1404 Hijria Shamsia), na kufikia dola milioni 675.
-
Araghchi: Sheria za kimataifa bado “zipo hai” licha ya kushambuliwa
Nov 18, 2025 11:26Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesisitiza ujumbe wa mkutano wa kimataifa kuhusu sheria za kimataifa, akisema mkutano huo umeonyesha dhamira ya Tehran ya kutetea haki mbele ya mashambulizi ya kigeni.
-
Iran yatoa mkono wa pole kwa India kufuatia kuaga dunia ajalini mahujaji wa nchi hiyo huko Saudi Arabia
Nov 18, 2025 11:24Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei ametuma salamu za rambirambi kwa familia za mahujaji wa ibada ya Umrah wa India waliofariki dunia katika ajali ya basi nchini Saudi Arabia.
-
Iran: Lazima IAEA idumishe uadilifu wa kiufundi na kutoegemea upande wowote kisiasa
Nov 18, 2025 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) lazima utimize maagizo uliyokabidhiwa ya kiufundi, ujiepushe na mielekeo ya kisiasa, na kukataa mashinikizo yanayotolewa na Marekani na washirika wake wa Ulaya.
-
Iran yalaani mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaondelezwa na Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi
Nov 17, 2025 09:16Iran imelaani vikali mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina pamoja na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.