Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran amuonya vikali Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135768-kamanda_mwandamizi_wa_jeshi_la_iran_amuonya_vikali_trump
Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amemuonya vikali Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 22, 2026 03:26 UTC
  • Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran amuonya vikali Trump

Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amemuonya vikali Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Admeli Habibollah Sayyari, Naibu Mratibu Mkuu wa Jeshi la Iran amesema hayo Jumatano ya jana, akijibu matamshi ya hivi karibuni ya Trump ya eti kutaka uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei ukomeshwe.

"Trump alikuwa amekosea kabisa," kamanda huyo amesisitiza, akikariri majibu makali kama hayo yaliyotolewa na maafisa wa ngazi za juu wa Iran kwa matamshi ya vitisho ya Rais wa Marekani dhidi ya Ayatullah Khamenei na Jamhuri ya Kiislamu.

Naye Jenerali Abolfazl Shekarchi, Msemaji wa Vikosi vya Jeshi la Iran siku ya Jumanne alipuuzilia mbali vitisho vya hivi karibuni vya Trump, akionya kwamba, hatua yoyote ya uadui itakayoelekezwa kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei itakabiliwa na kisasi kikubwa cha kijeshi.

"Trump anajua kwamba ikiwa mkono wa uchokozi utaelekezwa kwa Kiongozi wetu, hatutaukata tu mkono huo, na hii si kaulimbiu tu, lakini tutawasha moto kwenye ulimwengu wao na kuwaacha bila kuwa na pahali salama katika eneo," Jenerali Shekarchi amesisitiza.

Aidha haya yanajiri siku chache baada ya Rais Masoud Pezeshkian wa Iran kuonya pia kwamba, shambulio lolote dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu litakuwa tangazo la "vita kamili" na taifa la Iran.