Iran yatangaza idadi ya waliouawa katika ghasia zilizochochewa na maajinabi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135766-iran_yatangaza_idadi_ya_waliouawa_katika_ghasia_zilizochochewa_na_maajinabi
Wakfu wa Mashahidi na Maveterani wa Iran umetangaza katika taarifa kwamba, "katika vitendo vya hivi karibuni vya ugaidi vilivyoungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, watu 3117 walipoteza maisha yao, wakiwemo raia na maafisa usalama."
(last modified 2026-01-22T06:02:56+00:00 )
Jan 22, 2026 06:02 UTC
  • Iran yatangaza idadi ya waliouawa katika ghasia zilizochochewa na maajinabi

Wakfu wa Mashahidi na Maveterani wa Iran umetangaza katika taarifa kwamba, "katika vitendo vya hivi karibuni vya ugaidi vilivyoungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, watu 3117 walipoteza maisha yao, wakiwemo raia na maafisa usalama."

Taarifa ya wakfu huo imeeleza kuwa, "Hii ina maana kwamba, watu 2,427 miongoni mwao ama walikuwa vikosi vya usalama au raia wasio na hatia ambao waliuawa shahidi, na waliobaki walikuwa wahalifu au magaidi wenye silaha waliochochewa na maajinabi."

Wakfu wa Mashahidi na Maveterani wa Iran umebainisha kuwa, "Mashahidi hawa ni pamoja na maafisa usalama na makundi mbali mbali ya watu ambao walilengwa kwa kupigwa risasi na wataenda jinai za kigaidi; wakiwemo wapita njia na hata watoto wadogo wasio na hatia."

Baraza la Usalama wa Taifa la Iran limeeleza kuwa: Magaidi walishiriki katika "uhalifu wa mtindo wa Daesh," ikiwa ni pamoja na kukata watu vichwa, kuwachoma visu, na kuchoma watu moto wakiwa hai. Taarifa ya baraza hilo imesema, ghasia hizo pia zilisababisha uharibifu mkubwa kwenye masoko, maduka, benki, misikiti, hospitali, magari ya wagonjwa, vituo vya zimamoto, kliniki, na miundombinu ya umma.

Baraza holo limebainisha kwamba, matukio hayo yalianza kama maandamano ya amani ya wafanyabiashara na vikundi vya wajasiriamali kuhusu matatizo ya kiuchumi, ambapo Rais Masoud Pezeshkian alikutana na wawakilishi binafsi ili kusikiliza wasiwasi wao na kuwaagiza polisi kujizuia kabisa. Hata hivyo, ripoti hiyo imesema kwamba, mitandao ya machafuko yaliyopangwa iliingilia kati ili kuzuia kupatikana suluhu ya amani ya mgogoro huo, na kuanzisha mashambulizi ya silaha yaliyokusudiwa kusababisha vifo vya watu wengi na kuvuruga utulivu mijini.