Russia: Wananchi wa Iran wamesambaratisha njama za maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135802-russia_wananchi_wa_iran_wamesambaratisha_njama_za_maadui
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yalifadhiliwa waziwazi kutoka nje ya nchi.
(last modified 2026-01-23T04:07:04+00:00 )
Jan 23, 2026 04:07 UTC
  • Russia: Wananchi wa Iran wamesambaratisha njama za maadui
    Russia: Wananchi wa Iran wamesambaratisha njama za maadui

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yalifadhiliwa waziwazi kutoka nje ya nchi.

Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema hayo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari na kueleza kwamba, tunashuhudia hali ya kawaida nchini Iran. Aidha amebainisha kwamba, juhudi za maafisa wa Iran kudumisha sheria na utulivu, na muhimu zaidi, maandamano ya maelfu ya raia wa Iran ya kuunga mkono utaratibu wa kikatiba, uhuru, na mamlaka yya kujitawala nchi yamesambaratisha mipango ya uharibifu ya maadui ya kuivuruga nchi hii."

Maria Zakharova aliongeza: "Tunafurahi kwamba baada ya machafuko na vitendo vilivyotokana na msukumo kutoka nje ya Iran vilivyotokea katika siku za kwanza za Mwaka Mpya, sasa tunashuhudia hali ya kawaida ikitawala nchini Iran."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kusema kuwa, "Kundi la vikosi vya kigeni vyenye uadui vilivyojaribu kutekeleza hali wanayopenda ya mapinduzi ya rangi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vililazimika kukubali ukweli wa kurekebishwa kwa hali nchini Iran."

Zakharova pia alisema kwamba Russia kwa mara nyingine tena inaelezea mshikamano wake na watu wa Iran, akisema kwamba: Moscow iko katika mawasiliano ya karibu na ya mara kwa mara na washirika wake wa Kiirani. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alisema: Misheni za kidiplomasia za Russia nchini Iran zinafanya kazi kama kawaida.