Watu 95 wafariki dunia Zimbabwe baada ya kivuko kuzama kwenye Ziwa Kariba
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i140616-watu_95_wafariki_dunia_zimbabwe_baada_ya_kivuko_kuzama_kwenye_ziwa_kariba
Watu 95 wamefariki dunia nchini Zimbabwe, baada ya kivuko walichokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ziwa Kariba.
(last modified 2026-08-12T11:54:35+00:00 )
Aug 12, 2026 11:49 UTC
  • Watu 95 wafariki dunia Zimbabwe baada ya kivuko kuzama kwenye Ziwa Kariba

Watu 95 wamefariki dunia nchini Zimbabwe, baada ya kivuko walichokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ziwa Kariba.

Chombo hicho, ambacho kinatoa huduma za usafiri kati ya mji wa kaskazini wa Kariba na vijiji jirani, kilikumbwa na dhoruba kali, kabla ya kupinduka na kuzama ndani ya ziwa hilo.

"Shughuli za uokoaji zinaendelea na tutaendelea kutoa taarifa zaidi kadiri muda unavyokwenda,” imeeleza taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi la Zimbabwe siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo, baadhi ya abiria waliwahi kuokolewa, japo idadi yao haikuweza kufahamika mara moja.

Ziwa Kariba liko kwenye mpaka wa Zimbabwe na Zambia, yapata kilomita 300 kutoka mji mkuu wa Zimbabwe, Harare…/