Kamanda Mkuu wa Polisi ya Iran: Tutaendelea kuilinda Jamhuri ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135882-kamanda_mkuu_wa_polisi_ya_iran_tutaendelea_kuilinda_jamhuri_ya_kiislamu
Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan, Kamanda Mkuu wa Polisi ya Iran amesema kuwa wananchi na maafisa wa Iran watailinda Jamhuri ya Kiislamu hadi tone la mwisho la damu yao.
(last modified 2026-01-25T11:24:26+00:00 )
Jan 25, 2026 11:24 UTC
  • Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan
    Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan

Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan, Kamanda Mkuu wa Polisi ya Iran amesema kuwa wananchi na maafisa wa Iran watailinda Jamhuri ya Kiislamu hadi tone la mwisho la damu yao.

Kamanda Mkuu wa Polisi ya Iran amesema leo katika mkutano wa utekelezaji sheria kwamba maadui wanapasa kutambua kuwa taifa hili ni mashujaa wa Uislamu, na litasimama kidete, liko tayari kusabilia maisha kwa ajili ya kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu. 

Akizungumzia machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, Radan amesema, maadui wamejaribu kuibua mgawanyiko kati ya wananchi na mfumo tawala kwa kuzusha machafuko, lakini walishindwa kufikia lengo lao kutokana na kuwa macho na kujitolea kwa askari  usalama, wakiwemo polisi.

Brigedia Jenerali Ahmad Reza Radan ameashiria mchango na nafasi ya wananchi katika kusambaratisha fitna dhidi ya Iran na kuema kwamba, wananchi wa Iran wamekuwa bega kwa bega na Jamhuri ya Kiislamu kwa kipindi cha miaka 47 licha ya matatizo ya aina mbalimbali.

Ghasia kubwa zilizuka Iran tarehe 8 mwezi huu wa Januari baada ya makundi yanayoungwa mkono na kufadhiliwa na nchi ajinabi kufanye hujuma za kigaidi nchini, ikiwa ni pamoja na kuuwa raia wa kawaida na askari usalama na kuharibu mali za serikali na za watu binafsi. Hujuma hizo zilifanywa wakati wa maandamano yaliyoanza Desemba 28 kulalamikia gharama za maisha huku serikali ya Iran ikifanya mikutano na wawakilishi wa waandamanaji.