Uhalali wa kisheria wa Iran kujihami dhidi ya vitisho vya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135962-uhalali_wa_kisheria_wa_iran_kujihami_dhidi_ya_vitisho_vya_marekani
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima lieleze ukiukwaji uliofanywa na Marekani kwa uwazi na kwa majina yao halisi.
(last modified 2026-01-27T09:00:07+00:00 )
Jan 27, 2026 09:00 UTC
  • Uhalali wa kisheria wa Iran kujihami dhidi ya vitisho vya Marekani
    Uhalali wa kisheria wa Iran kujihami dhidi ya vitisho vya Marekani

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima lieleze ukiukwaji uliofanywa na Marekani kwa uwazi na kwa majina yao halisi.

Amir Saeed Iravani, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, amesema hayo akijibu vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Iran na kueleza kwamba, "Marekani inatishia nchi huru kila mara kwa mashambulizi dhidi ya mamlaka ya ardhi za kigeni.

Iravani ameongeza kuwa: "Trump anaitishia Iran hadharani na mara kwa mara kwa kutumia nguvu na uingiliaji kati wa kijeshi."

Katika miaka ya hivi karibuni, mvutano unaotokana na vitisho vya Marekani na hatua za upande mmoja dhidi ya baadhi ya nchi, ikiwa ni pamoja na Iran, umeleta tena suala la kuheshimiwa kanuni za sheria za kimataifa na kuzingatiwa jukumu la Umoja wa Mataifa kwa nchi huru zinazopinga maamuzi ya upande mmoja ya Ikulu ya White House.

Matamshi ya mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, ambayo yanasisitiza hitajio la jibu dhahiri kutoka kwa Baraza la Usalama kwa "ukiukwaji wa Marekani," ni muktadha unaofaa wa kuchunguza vipimo vya kisheria, kisiasa, na kitaasisi vya suala hili.

Mfumo wa kimataifa umejengwa juu ya kanuni zinazolenga kudumisha amani, kuzuia vita, na kuhakikisha heshima kwa mamlaka ya kujitawala mataifa. Mkataba wa Umoja wa Mataifa unakataza tishio au matumizi ya nguvu. Hata hivyo, katika utendaji, tabia ya mataifa makubwa, hasa Marekani, imekuwa mada ya mjadala na changamoto kila mara. Taarifa za hivi karibuni za mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa zinaonyesha mfano wa changamoto hizi na zinaangazia haja ya  kupitia upya jukumu na ufanisi wa taasisi za kimataifa.

Iran imetangaza kuwa, imejiandaa kikamilifu kukabiliana na uchokozi wa aina yoyote kutoka kwa adui

 

Kutoa vitisho vya kijeshi, hata kama hakutatekelezwa, kunaweza kuwa ukiukaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa mtazamo wa sheria za kimataifa. Mwakilishi huyo wa Iran alisisitiza katika maelezo yake kwamba, maafisa wa Marekani, akiwemo Rais Donald Trump, wametishia Iran mara kwa mara kwa hatua za kijeshi. Vitisho hivyo, vikitolewa bila idhini ya Baraza la Usalama au bila kuwa na msingi wa kujilinda, vinapingana na kanuni za msingi za sheria za kimataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Kwa hivyo, tishio lolote la matumizi ya nguvu lazima lishughulikiwe katika baraza hili. Mwakilishi wa Iran amesisitiza kwamba Baraza la Uusalama lazima "liite ukiukwaji wa Marekani kwa jina lake halisi."

Mojawapo ya vikwazo vikuu katika njia hii ni muundo wa Baraza la Usalama na kuwepo kwa haki ya kura ya turufu. Muundo huu hufanya mataifa makubwa kuwa salama kutokana na usimamizi mzuri wa baraza hilo. Suala hili limekosolewa mara kwa mara na nchi mbalimbali na limeimarisha mjadala wa kurekebisha muundo wa Baraza la Usalama.

Kuzingatia kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kuzuia tishio la kutumia mabavu, na kuhakikisha kutoegemea upande wowote kwa taasisi za kimataifa ni muhimu kwa ajili ya kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Wakati huo huo, Baraza la Usalama lazima lichukue jukumu kubwa zaidi na kuepuka utekelezaji wa sheria kwa njia ya ubaguzi. Ni katika hali hii ndipo tunaweza kuwa na matumaini ya ufanisi na uhalali wa mfumo wa kimataifa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza mara kwa mara "haki yake ya asili na kisheria" ya kukabiliana na kujilinda dhidi ya vitisho kutoka kwa Marekani. Msimamo huu unategemea kanuni za sheria za kimataifa, hasa Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kwa mtazamo wa maafisa wa Iran, vitisho vya Marekani ni ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na Iran inaruhusiwa kujibu vitisho hivi kwa kuzingatia haki ya kujilinda, kanuni ya uhuru na mamlaka ya kitaifa, na marufuku ya matumizi ya mabavu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inasisitiza kanuni ya uhuru na mamlaka ya kitaifa na hitajio la kudumisha uhuru wake wa kisiasa, na inaona vitisho vya Marekani kama changamoto kwa kanuni hizi. Zaidi ya hayo, rekodi ya kihistoria ya uingiliaji kati wa kijeshi wa Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia, kwa mtazamo wa Iran, inafanya vitisho vya sasa kuonekana halisi na muhimu, na inaimarisha udharura wa kupitisha sera za kuzuia.

Kwa muhtasari, kwa mtazamo wa viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kukabiliana na vitisho vya Marekani si haki tu, bali pia ni wajibu wa kulinda usalama wa taifa, umoja wa ardhi, na uhuru wa nchi; haki inayotambuliwa na mkataba wa Umoja wa Mataifa na inayoweza kutetewa ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa.