-
Ufaransa na nchi nyingine 9 kuitambua rasmi Palestina
Sep 20, 2025 11:48Katika hatua ya kihistoria, Ufaransa na nchi nyingine tisa zimetangaza kuwa zitalitambua rasmi taifa huru la Palestina.
-
Amnesty International: Kura ya turufu ya Marekani ni taa ya kijani kwa mauaji ya kimbari huko Gaza
Sep 20, 2025 11:22Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, limekosoa vikali kura ya turufu ya Marekani dhidi ya azimio la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, likitaja hatua hiyo kama uungaji mkono wa moja kwa moja kwa jinai za kutisha za Israel.
-
Guterres: Ulimwengu haupaswi kutishwa na vitisho vya Israel kuhusu Palestina
Sep 20, 2025 11:18Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba vitisho vya Israel havipaswi kuzuia kutambuliwa rasmni kwa taifa la Palestina.
-
Brazil yaungana rasmi na Afrika Kusini katika kesi ya mauaji ya halaiki dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)
Sep 20, 2025 07:37Brazil imewasilisha rasmi ombi la kujiunga katika kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Israel kuhusu vita vinavyoendelea tangu Oktoba 2023 ambavyo vinatambuliwa na wengi kuwa ni vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
-
Duru za Uturuki: Erdogan amefanya mazungumzo ya siri Istanbul na mwana wa kiume wa Trump
Sep 19, 2025 11:07Mwana mkubwa wa kiume wa Rais Donald Trump wa Marekani na ujumbe alioandamana nao wiki iliyopita walikutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul wiki katika ziara ambayo haikutangazwa. Hayo yameripotiwa na duru zilizodai kuwa na uelewa wa suala hilo.
-
Taliban yamjibu Trump: Tunaweza kuzungumza, lakini Marekani haitaruhusiwa kuwepo tena kijeshi Afghanistan
Sep 19, 2025 11:05Serikali ya Afghanistan inayoongozwa na Taliban imetupilia mbali wito wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutaka jeshi la nchi hiyo lirejee Afghanista na kupatiwa tena kambi ya jeshi la anga ya Bagram.
-
Marekani yatumia kura ya veto kupinga azimio la kusitisha vita Gaza
Sep 19, 2025 03:56Marekani imetumia kura turufu kuzuia kupasishwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka usitishwaji vita Gaza, kuwezesha ufikaji wa misaada ya kibinadamu na kuachiliwa kwa mateka.
-
Mayahudi wa Othodoksi waanza kuandamana New York dhidi ya Netanyahu kabla hajaelekea UN
Sep 18, 2025 10:13Mamia ya Wayahudi wa madhehebu ya Othodoksi wamefanya maandamano katika jiji la New York kupinga ushiriki wa waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa itakayofanyika wiki ijayo.
-
Uingereza inamngojea Trump amalize ziara yake ndipo itangaze kulitambua Dola la Palestina
Sep 18, 2025 10:12Uingereza itaitambua rasmi Palestina kama Dola mwishoni mwa wiki hii baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhitimisha ziara yake ya kiserikali nchini humo. Hayo yamefichuliwa na gazeti la The i Paper likivinukuu vyanzo vya serikali.
-
Financial Times: EU inapanga kuzitumia yuro bilioni 170 fedha za Russia inazozishikilia
Sep 18, 2025 10:11Gazeti la Financial Times limeripoti kuwa Umoja wa Ulaya (EU) umeamua kutekeleza mpango wa kuzitumia yuro bilioni 170 milki za Russia inazozishikilia kurudisha "mikopo ya fidia" kwa Ukraine.