-
Putin: Russia na China ni watetezi wa ukweli wa kihistoria
May 08, 2025 10:50Moscow na Beijing zinaendelea kuwa watetezi thabiti wa ukweli wa kihistoria na zikikumbuka idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha katika nchi zao wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Rais Vladimir Putin wa Russia ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais Xi Jinping wa China.
-
Pakistan: Tutalipiza kisasi cha mashambulio ya makombora ya India yalioua 31
May 08, 2025 07:05Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif amesema nchi hiyo "italipiza kisasi cha damu za mashahidi wetu wasio na hatia" baada ya watu wasiopungua 31 kuripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulio ya India kwenye mkoa wa Punjab na Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan.
-
Mashirika 113 ya haki za binadamu yatoa wito kwa Baraza la Usalama kuiwekea Israel vikwazo
May 08, 2025 03:04Mitandao na mashirika 113 ya kutetea haki za binadamu duniani kote yamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya kimataifa kwa utawala ghasibu wa Israel ili kukomesha mauaji ya kimbari na njaa katika Ukanda wa Gaza, na kuondoa kukamilifu mzingiro wa eneo hilo.
-
Kurudi nyuma Marekani katika vita ilivyoanzisha dhidi ya Yemen; matunda ya Muqawama wa Wayemen
May 08, 2025 02:23Msemaji wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah, Muhammad Abdul Salam amesema, Yemen haitaiacha Ghaza peke yake licha ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita, na kwamba Marekani ndiyo iliyoomba kusitishwa mapigano.
-
Guterres ataka India na Pakistan zisitishe operesheni za kijeshi
May 07, 2025 12:44Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kuhusu operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la India kwenye mstari wa usimamizi na mpaka wake wa kimataifa na Pakistan.
-
Kansela mpya wa Ujerumani aionya Marekani iache kuingilia siasa za ndani
May 07, 2025 12:28Kansela mpya wa Ujerumani, Friedrich Merz, leo Jumatano ameionya Marekani dhidi ya kuingilia siasa za ndani za nchi yake.
-
India yaishambulia Pakistan kwa makombora
May 07, 2025 07:12India imeishambulia Pakistan na hivyo kuibua wasiwasi wa kuzuka vita baina ya mataifa hayo jirani.
-
Russia yaituhumu Ulaya na NATO kuwa zinajiandaa kwa makabiliano ya moja kwa moja ya kijeshi
May 07, 2025 06:35Katibu wa Baraza la Usalama la Russia, Sergei Shoigu, amelituhumu shirika la kijeshi la nchi za Magharibi, NATO na Umoja wa Ulaya kuwa zinaandaa mzozo wa moja kwa moja wa kijeshi na Moscow.
-
Umoja wa Ulaya na juhudi za kupata washirika wapya wa kibiashara
May 07, 2025 02:19Vitendo vya Rais Donald Trump wa Marekani hususan kuanza kwa vita vya kibiashara na dunia ambavyo vimesababisha machafuko katika mfumo wa uchumi na biashara wa kimataifa, vimeufanya Umoja wa Ulaya kutaka kupanua na kuimarisha uhusiano wake na nchi za Bahari ya Pasifiki (Trans-Pacific).
-
Uhispania: Tutaendelea kuisaidia UN kifedha kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na Israel Ghaza
May 06, 2025 06:40Uhispania itachangia yuro 500,000 (zaidi ya $560,000) kusaidia uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita unaowezekana kuwa umefanywa huko Ghaza. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Albares.