-
Uhispania: Tutaendelea kuisaidia UN kifedha kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na Israel Ghaza
May 06, 2025 06:40Uhispania itachangia yuro 500,000 (zaidi ya $560,000) kusaidia uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita unaowezekana kuwa umefanywa huko Ghaza. Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Albares.
-
Wataalamu wa Vatican: Papa ajaye aliunganishe Kanisa kutokana na mpasuko mkubwa uliopo
May 06, 2025 06:15Wakati Kanisa Katoliki linajiandaa kwa mkutano wa kumchagua Papa mpya utakaoanza kesho Jumatano, wachambuzi wa Vatican wanasema, makadinali wako chini ya mashinikizo ya kumchagua papa mwenye uwezo wa kuziba mgawanyiko unaoendelea kukua kati ya pande mbili kuu za wanamageuzi na wahafidhina ndani ya Kanisa hilo.
-
Vita na Trump: Sasa Ulaya yatafuta washirika wa Asia na Pasifiki
May 06, 2025 02:43Hatua ya rais wa Marekani ya kuvuruga mfumo wa uhusiano wa kimataifa, imeulazimisha Umoja wa Ulaya kuamua kuimarisha uhusiano wake na nchi za Asia na Pasiriki kupitia jumuiya kama Trans-Pacific.
-
Kukabiliana mataifa ya Amerika Kusini na vita vya ushuru vya Trump
May 05, 2025 13:24Wanachama wa Soko la Pamoja la Amerika Kusini (Mercado Común del Sur) wameongeza idadi ya bidhaa zisizo na ushuru kwa bidhaa zinazoangizwa kutoka nje ya jumuiya ya kikanda, katika hatua muhimu dhidi ya vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
-
Mkuu wa zamani wa CIA: Tuliipatia Ukraine silaha za kiasi cha 'kuvuja damu', si 'kushinda vita'
May 05, 2025 11:39Afisa mwandamizi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA Ralph Goff amesema nchi hiyo iliweka makusudi vizuizi vya msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili kuiacha nchi hiyo "ivuje damu" badala ya "kushinda" vita kati yake na Russia.
-
Russia yasisitiza: Iran iko sahihi kabisa, haki za kinyuklia za kila nchi haziwezi kupingwa
May 05, 2025 10:57Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa yenye makao yao mjini Vienna ametilia nguvu msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu haki yake ya kumiliki mzunguko kamili wa fueli ya nyuklia na kusisitiza kwamba haki za kinyuklia zilizonazo nchi wanachama wa Mkataba wa Kuzuia Uenezaji Silaha za Atomiki (NPT) haziwezi kupingwa wala kukanushwa.
-
Rais wa Mexico amjibu Trump: Tuko tayari kwa ushirikiano, lakini hatukubali kamwe 'kutiishwa' na US
May 05, 2025 10:16Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum amekataa pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kupeleka wanajeshi ndani ya ardhi ya nchi hiyo kupambana na magenge ya madawa ya kulevya na akasisitiza kwamba, wakati Mexico imeweka mlango wazi kwa ushirikiano, haitakubali kamwe "kutiishwa" kwa Washington.
-
Putin: Tunatumai hatutalazimika kutumia silaha za nyuklia Ukraine
May 05, 2025 02:22Rais wa Russia, Vladimir Putin amesema kufikia sasa, udharura wa kutumia silaha za nyuklia nchini Ukraine haujajitokeza, na kwamba anatumai hautatokea.
-
Makosa 6 makubwa ya kimkakati ya Marekani kuhusu Iran
May 05, 2025 02:22Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran, Marekani ikiwa kiongozi wa nchi za Magharibi, muda wote imekuwa ikilifanyia uadui taifa la Iran katika kipindi cha miaka 46 sasa ikiwa ni pamoja na kuliwekea vikwazo vikubwa kupindukia. Hata hivyo Washington imeshindwa kufikia malengo yake dhidi ya Iran.
-
Trump akosolewa baada ya kuchapisha picha yake akiwa amevaa vazi kama la Papa
May 04, 2025 07:46Rais wa Marekani, Donald Trump, anakabiliwa na shutuma baada ya kuchapisha picha iliyotengenezwa kwa kutumia akili mnemba (AI) inayomuonyesha akiwa amevalia kama papa wa Kanisa Katoliki kwenye jukwaa lake la Truth Social.