Waislamu waadhimisha siku ya kuzaliwa Mwokozi wa Akheri Zamani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i136236-waislamu_waadhimisha_siku_ya_kuzaliwa_mwokozi_wa_akheri_zamani
Waislamu wa madhehebu ya Shia katiika maeneo mbalimbali ya dunia Leo Jumatano mwezi 15 Shaaban wanaadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam wa Zama, Imam Mahdi AS, Imam wa 12 wa katika kizazi cha Mtume wetu Muhammad (SAW).
(last modified 2026-02-04T04:27:48+00:00 )
Feb 04, 2026 04:27 UTC
  • Waislamu waadhimisha siku ya kuzaliwa Mwokozi wa Akheri Zamani

Waislamu wa madhehebu ya Shia katiika maeneo mbalimbali ya dunia Leo Jumatano mwezi 15 Shaaban wanaadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam wa Zama, Imam Mahdi AS, Imam wa 12 wa katika kizazi cha Mtume wetu Muhammad (SAW).

Kwa mnasaba huo adhimu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo imeungana na maeneo mengine ya duniia kuadhimisha kuzaliwa Imam wa Zama, Mahdi (AF).

Maeneo tofauti ya Iran ya Kiislamu hususan katika miji mitakatifu ya Mash'had na Qum tangu jioni ya jana ilighariki katika sherehe za maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Mwokozi wa ulimwengu, Imam Zama, Mahdi (AS).

Kwa kawaida, katika siku ya maadhimisho ya kuzaliwa Imam Mahdi AS, Waislamu wa Iran hukusanyika kwenye maeneo matakatifu, misikitini, kumbi za masuala ya kijamii na hata mitaani kufanya sherehe mbalimbali na hasa kuomba dua na kusoma kasida za kumsifu Mtume (saw) na Ahlibaiti zake watoharifu.

Kwa mujibu wa wanahistoria, Imam Mahdi (AS), mwana wa Imam Hasan al Askari (as) alizaliwa huko Samarrah nchini Iraq mwezi 15 Shaaban mwaka 255 Hijria..

Yeye ni mwana mpendwa wa Imam Hassan Askari AS ambaye ni mmoja wa wajukuu wa Mtume Muhammad SAW. Miongoni mwa lakabu mashuhuri za Imam huyo wa Zama ni Mahdi, al Qaim.

Atakapodhihiri duniani, ataijaza dunia kwa uadilifu na usawa baada ya kujaa dhulma na uonevu. Siku ya kuzaliwa mtukufu huyo huadhimishwa nchini Iran kama Siku ya Waliodhulumiwa Duniani. 

Tunatoa mkono wa kheri na baraka kwa wapenda haki wote hasa wafuasi wa kweli wa Ahlul Baiti wa Bwana Mtume Muhammad SAW kwa mnasaba wa kuchomoza nuru hiyo ya haki.