-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu utumiaji wa mada zilizopigwa marufuku dhidi ya raia wa Iran
Aug 01, 2026 11:26Maripota wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa taarifa ya pamoja, wakisema kuwa raia 3,375 wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya kikatili ya Marekani na Israel (wakiwemo wanawake wapatao 500), na kutoa wito wa kuwajibishwa Marekani na Israel kwa uhalifu wao wa kivita, hasa kuhusu janga la shule ya msingi ya Minab.
-
Meya wa Moscow: Zaidi ya droni 6,000 za Ukraine zililenga mji mkuu wa Russia mwezi Julai
Aug 01, 2026 11:18Zaidi ya ndege zisizo na rubani (droni) 6,000 za Ukraine ziliulenga mji mkuu wa Russia, Moscow mwezi Julai mwaka huu. Haya yameelezwa na, Meya wa Moscow, Sergey Sobyanin.
-
Kwa nini Nguvu ya Marekani Inaelekea Ukingoni?
Aug 01, 2026 06:08Miongo mitatu baada ya operesheni ya "Desert Storm," mtazamo ndani ya duru za kimkakati za Marekani ni kwamba zama za nguvu na utawala usio na mpinzani wa Washington zimefikia ukingoni. Vita na Iran vimethibitisha kuwa mwenendo wa mabadiliko katika uwiano wa nguvu na kupungua kwa uwezo wa Marekani wa kuzuia vitisho (deterrence credibility) ndani ya mfumo wa dunia umeanza kushika kasi.
-
Karibu nusu ya Wamarekani wanataka Netanyahu akamatwe licha ya propaganda za mamilioni ya dola
Jul 31, 2026 03:31Karibu nusu ya Wamarekani wanataka waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe licha ya propaganda zinazofanywa na utawala huo wa kizayuni ambazo zimeugharimu mamilioni ya dola.
-
Amnesty International: India inashiriki katika mauaji ya kimbari ya Gaza
Jul 31, 2026 03:20Katika ripoti mpya iliyotolewa jana, Julai 30, Amnesty International imefichua data za forodha kuhusu usafirishaji kutoka India kuelekea Israel, ikisema kwamba New Delhi imeendelea kusafirisha vipuri vya zana za kijeshi, risasi na vifaa kwa makampuni ya Israel licha ya hatari iliyo wazi ya silaha hizo kutumika katika mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.
-
Karibu nusu ya Wamarekani wanataka Netanyahu akamatwe licha ya propaganda za mamilioni ya dola
Jul 30, 2026 10:18Karibu nusu ya Wamarekani wanataka waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe licha ya propaganda zinazofanywa na utawala huo wa kizayuni ambazo zimeugharimu mamilioni ya dola.
-
UNHCR yaonya juu ya ukandamizaji wa haki za wakimbizi
Jul 30, 2026 04:04Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema haki za waomba hifadhi ulimwenguni zinakabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa. Hayo yameelezwa wakati shirika hilo likiadhimisha miaka 75 ya kupitishwa kwa Mkataba wa Wakimbiuzi.
-
Zakharova: Shambulio la Ukraine dhidi ya meli ya Iran lilikuwa kitendo cha wazi cha ugaidi
Jul 30, 2026 04:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameikosoa vikali serikali ya Kyiv, akisisitiza kuwa shambulio la Ukraine dhidi ya meli ya Iran lilikuwa mfano halisi wa kitendo cha kigaidi.
-
Katibu Mkuu wa UN: Mkataba kuhusu wakimbizi si wa kupuuzwa
Jul 29, 2026 02:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi zote wanachama kuhuisha dhamira yao ya kutekeleza Mkataba wa Wakimbizi wa mwaka 1951, akisema haki ya watu wanaokimbia mateso kutafuta hifadhi inazidi kutiliwa shaka, kuwekewa vikwazo au kunyimwa.
-
Licha ya ushahidi wa UN, serikali ya UK yakataa kutambua mauaji ya kimbari ya Ghaza
Jul 29, 2026 02:23Serikali mpya ya Uingereza imekataa wito uliotolewa wabunge 80 na wenzao wa kuyatambua mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza, kuuwekea utawala huo wa kizayuni vikwazo kamili vya silaha na kuanzisha vikwazo kamili dhidi ya utawala huo ghasibu.