-
Licha ya ushahidi wa UN, serikali ya UK yakataa kutambua mauaji ya kimbari ya Ghaza
Jul 29, 2026 02:23Serikali mpya ya Uingereza imekataa wito uliotolewa wabunge 80 na wenzao wa kuyatambua mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza, kuuwekea utawala huo wa kizayuni vikwazo kamili vya silaha na kuanzisha vikwazo kamili dhidi ya utawala huo ghasibu.
-
Wabunge wa US waanza kuchunguza ufisadi kuhusu FIFA na uhusiano wa Infantino na Trump
Jul 28, 2026 13:56Mbunge mmoja nchini Marekani wa chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi la nchi hiyo ametangaza kuanzishwa uchunguzi kuhusu shirikisho la soka duniani FIFA, akiongeza kuwa inawezekana kukawepo na uhusiano kati ya shirikisho hilo na serikali ya Rais wa Marekani Donald Trump.
-
Wakati Trump Anapokiuka Hata Ahadi Alizotoa kwa Washirika wake wa Kikanda!
Jul 28, 2026 08:18Rais Donald Trump wa Marekani amekiuka ahadi yake ya awali kwa Saudi Arabia kwa kutangaza masharti mapya ya utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya nchi hizo mbili.
-
Putin: Maadui wa Russia wamejielekeza katika mbinu za wazi za kigaidi
Jul 28, 2026 03:50Rais wa Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa maadui wa nchi hiyo wameamua kutumia mbinu za wazi za kigaidi, na kwamba Moscow itatimiza malengo yake yote ya kijeshi katika vita vya Ukraine na iko tayari kutoa jibu kwa hatua yoyote ya uhasama.
-
Maelfu Waandamana Jakarta kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza
Jul 27, 2026 08:41Maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuuu wa Indonesia Jakarta kulaani mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Malaysia yasisitiza msimamo wake wa kuendelea kuwafukuza Waisraeli
Jul 26, 2026 02:51Waziri wa Ulinzi wa Malaysia, Mohamed Khaled Nordin, amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo itaendelea kuwafukuza raia wa Israel kutoka katika ardhi ya Malaysia, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya sera ya muda mrefu ya Kuala Lumpur ya kutoutambua utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mwendesha-mashtaka wa ICC Karim Khan aondolewa kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono
Jul 25, 2026 02:58Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) umepiga kura ya kumwondoa Mwendesha Mashtaka Karim Khan kufuatia madai ya utovu wa nidhamu wa kingono; timu yake ya wanasheria imethibitisha hayo, huku ikidokeza kuwa hatua hiyo ilikuwa ya "kisiasa".
-
Mamdani ataka Marekani imkamate Netanyahu kwa uhalifu wa kivita
Jul 23, 2026 02:46Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, amemtaja Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuwa ni mhalifu wa kivita, na kuitaka serikali ya Marekani kutekeleza hati ya kukamatwa kwake iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iwapo atatia mguu katika ardhi ya Marekani.
-
Vyombo vya habari Marekani: Trump anataka kumteua rais wa FIFA kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Jul 22, 2026 10:19Rais wa Marekani, Donald Trump, anataka kumteua Rais wa FIFA, Gianni Infantino katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
-
Uholanzi yatangaza kususia bidhaa zinazotoka Israel
Jul 22, 2026 09:47Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, serikali ya Uholanzi imeamua kupiga marufuku uingizaji, ununuzi na uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa katika maeneo ya vitongozi haramu vya walowezi wa utawala wa Kizayuni.