John Mearsheimer: Hakuna nguvu duniani yenye uwezo wa kuishinda Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138634-john_mearsheimer_hakuna_nguvu_duniani_yenye_uwezo_wa_kuishinda_iran
Profesa wa sayansi ya siasa na mtaalamu wa nadharia ya mahusiano ya kimataifa amesema kuwa: Wakati Marekani na Israel zimeshindwa kuishinda Iran kwa kutumia nguvu zao zote, katika kipindi cha siku 40 za mashambulizi ya anga, hakuna nguvu nyingine duniani yenye uwezo wa kufanya hivyo.
(last modified 2026-05-26T02:55:01+00:00 )
May 26, 2026 02:53 UTC
  • John Mearsheimer
    John Mearsheimer

Profesa wa sayansi ya siasa na mtaalamu wa nadharia ya mahusiano ya kimataifa amesema kuwa: Wakati Marekani na Israel zimeshindwa kuishinda Iran kwa kutumia nguvu zao zote, katika kipindi cha siku 40 za mashambulizi ya anga, hakuna nguvu nyingine duniani yenye uwezo wa kufanya hivyo.

John Mearsheimer, profesa wa sayansi ya siasa na mtaalamu wa mahusiano ya kimataifa wa Marekani, amesema: Kwa miaka mingi lobi za Israel zimekuwa zikiahidi mabadiliko ya utawala nchini Iran, lakini ukweli ni kwamba Iran iko imara katika nafasi yake.

Mearsheimer ameongeza kuwa: Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeshirikiana na Marekani na Israel katika mashambulizi dhidi ya Iran na inaelekea vitani; lakini haina ubavu wa kuingia kwenye mchezo huo na wala haiwezi kusimama pekee yake dhidi ya Iran.

Profesa huyo wa sayansi ya siasa amesema: Ikiwa UAE itaingia vitani, Wairani watalenga kwa urahisi mitambo yao ya kusafisha maji ya chumvi na miundombinu ya nishati na kuharibu kabisa nchi hiyo. Amesisitiza kwamba UAE inapaswa kufikia makubaliano mara moja na Iran.