Naim Qassem: Mradi wa kuangamiza Iran na Muqawama umefeli
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i139334-naim_qassem_mradi_wa_kuangamiza_iran_na_muqawama_umefeli
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwamba, mradi wa kuisambaratisha Iran na muqawama katika eneo hilio la Asia Magharibi umeshindwa na kugonga mwamba.
(last modified 2026-06-22T14:14:57+00:00 )
Jun 22, 2026 09:06 UTC
  • Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah
    Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwamba, mradi wa kuisambaratisha Iran na muqawama katika eneo hilio la Asia Magharibi umeshindwa na kugonga mwamba.

Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria kushindwa mradi wa kusambaratisha muqawama katika eneo hili na kusema kwamba, licha ya takriban mashambulizi ya anga 10,000 katika vita vya "Al-Asf al-Maakul" nchini Lebanon, muqawama umeendelea kubakia imara na madhubuti.

Aidha amebainisha kwamba, mradi wa Marekani na Israel wa kusambaratisha Mhimili wa Muqawama umeshindwa na kusisitiza kwamba, sasa tumeingia katika awamu mpya, ambayo inaweza kuitwa 'matokeo ya kushindwa mradi wa Marekani-Israel'.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amezungumzia pia hali ya mambo nchini Lebanon na kueleza kwamba: "Uvamizi umeshindwa na haujafikia malengo yake, lakini Waisrael bado wanategemea kutokea mabadiliko ya hali ya mambo."

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Hizbullah amesema, "Iran imejitokeza ikiwa imara zaidi baada ya kujitolea mhanga kwa wingi na imethibitisha kuwa, katu haitafumbia macho haki zake."

Sheikh Naim Qassem, amebainisha kwamba, Marekani lazima isitishe mradi wa Israel, na akaongeza kusema kuwa, "Nina hakika kwamba Israel itaporomoka na kusambaratika kutoka ndani, na kile inachofanya ni dhulma kubwa dhidi ya ubinadamu."

Kuhusiana na usitishaji vita nchini Lebanon Sheikh Naim Qassem amesema: "Hatutavumilia ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na tutaukabili, tukichukua hatua zinazofaa.