-
Iran: Trump anaongopa kudai kuwa tumeomba tufanye mazungumzo
Jul 08, 2025 13:14Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha vikali matamshi ya Rais wa Marekani, Donald Trump kwamba Tehran imeomba kufanyike mazungumzo, ikiikashifu Washington kwa kubuni madai yasiyo na msingi ili kuficha kushindwa kwake.
-
Meja Jenerali Mousavi: Jeshi la Iran lilikabiliana na uvamizi wa Israel, US kwa 'nguvu kamili'
Jul 08, 2025 10:21Kamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Iran amesema Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu vilikabiliana na uvamizi wa Israel na Marekani kwa nguvu na uwezo kamili wa kijeshi wakati wa mashambulizi ya kichokozi ya mwezi uliopita ya Tel Aviv na Washington.
-
Rais Pezeshkian: Israel ilijaribu kuniua, siogopi kifo
Jul 08, 2025 04:24Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kuwa utawala haramu wa Israel ulitekeleza jaribio la kumuua wakati wa vita hivi karibuni. Aidha amesisitiza kuwa Iran “haina tatizo” kurejea kwenye mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia, lakini anasisitiza kuwa lazima kuwe na dhamana kwamba Israel haitafanya tena shambulio wakati wa mazungumzo ya kidiplomasia, kama ilivyofanya mwezi uliopita.
-
Araghchi:Uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran ni ukiukaji wa sheria za kimataifa
Jul 08, 2025 04:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Dkt. Seyyed Abbas Araghchi, amelaani vikali mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akiyataja kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa, Hati ya Umoja wa Mataifa, na Kanuni za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Israel inataka kuanzisha tena vita, Iran iko kwenye hali ya utayari kamili
Jul 07, 2025 13:46Chanzo kimoja cha habari cha Iran kimeiambia chaneli ya Press TV kwamba utawala wa kizayuni wa Israel unataka vita viendelee na Rais wa Marekani Donald Trump anaonekana kuunga mkono suala hilo.
-
Iran yalaani mashambulizi mapya ya Israel dhidi ya Yemen
Jul 07, 2025 08:47Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali mashambulizi mapya ya utawala wa Israel dhidi ya miundombinu ya kiraia ya Yemen na kuendelea kutoadhibiwa kwa Tel Aviv kutokana na ukatili unaofanyika kwa msaada endelevu wa Marekani.
-
Jenerali Shekarchi: Iran itatoa jibu la kuponda zaidi iwapo Israel itaishambulia tena
Jul 07, 2025 08:02Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran ameonya kuwa, Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kufanya mashambulizi yenye nguvu na ya maangamizi zaidi dhidi ya vitendo vyovyote vya kichokozi vitakavyofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya taifa hili.
-
Mshauri wa IRGC: Uwezo mkubwa wa ulinzi wa Iran bado haujaonyeshwa
Jul 07, 2025 03:03Mshauri mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Brigedia Jenerali Ebrahim Jabbari amesema kuwa silaha, zana za kijeshi na vituo vingi vya ulinzi vya Iran bado havijaonyeshwa na kuwekwa paruwanja.
-
Iran: Ugaidi wa kijeshi wa Israel ni pigo kwa diplomasia, NPT
Jul 06, 2025 14:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amelaani uvamizi na hujuma zilizofanywa hivi karibuni na Marekani na Israel dhidi ya Iran, na kuzieleza kuwa pigo kubwa kwa diplomasia, utawala wa sheria na Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Umuhimu wa vikao na mashauriano aliyofanya Rais wa Iran katika mkutano wa ECO
Jul 06, 2025 09:36Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambaye alikuweko nchini Jamhuri ya Azerbaijan alikohudhuria mkutano wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi, ECO, alikutana na viongozi wa nchi zingine wanachama wa jumuiya hiyo, wakabadilishana Mawazo kuhusu matukio ya kikanda na namna ya kupanua ushirikiano kati ya pande mbili.