Pars Today
Leo Jumamosi tarehe 12 mwezi Bahman sawa na Februari Mosi ni siku ya kuanza alfajiri kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Leo Jumatatu tarehe 11 Februari 2019 ambayo imesadifiana na tarehe 22 Bahman 1397 kwa mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia, ni siku ambayo zimefikia kileleni sherehe za miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mamilioni ya wananchi Waislamu wa Iran wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mfalme wa Oman Qaboos bin Said amemtumia ujumbe wa pongezi Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mufti Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Kisuni nchini Iraq ameyasifu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa, yamekuwa na taathira chanya katika Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla.
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana sifa za kipekee. Umoja wa kitaifa na utukufu wa Uislamu ambayo ni misingi muhimu ya dola la kimataifa la Imam Mahdi (af) ni baadhi ya sifa za mapinduzi hayo.
Wananchi wa Iran wameanza sherehe za Alfajiri Kumi katika kona zote za nchi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 39 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran ambayo yaliupindua utawala wa kitaghuti wa Kipahlavi uliokuwa unaungwa mkono kila upande na Marekani.