-
Rais Rouhani: Kuuliwa shahidi Soleimani kutazidisha azma ya Iran ya kupambana na ubeberu wa Marekani
Jan 03, 2020 07:22Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuuliwa shahidi Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi al Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) kutazidisha mara dufu azma ya Iran na mataifa mengine huru ya kusimama kidete kupambana na ubeberu wa Marekani na kulinda thamani na maadili ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Kisasi kikali kinawasubiri waliomuua shahidi Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 06:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kutokana na kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qassem Solaimani na kusema kuwa: Kisasi kikali kinawasubiri watenda jinai ambao mikono yao michafu imemwaga damu yake na mashahidi wengine katika shambulizi la usiku wa kuamkia leo.
-
Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes wauawa shahidi na helikopta ya Marekani, uwanja wa ndege wa Baghdad
Jan 03, 2020 03:28Duru za habari zinaripoti kuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.