-
Katibu Mkuu wa Ansarullah: Macron ni kikaragosi kinachochezeshwa na Wazayuni
Oct 29, 2020 23:01Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema rais Emmanuel Macron wa Ufaranmsa ni kikaragosi kinachochezeshwa na Wazayuni kichukue hatua za kuutusi na kuuvunjia heshima Uislamu.
-
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Ufaransa, awataka wamhoji Macron kwa nini anamtusi Mtume wa Mungu kwa jina la uhuru wa maoni?
Oct 29, 2020 07:52Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewatumia ujumbe vijana wa Ufaransa akiwataka wamhoji Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron kwa nini kwa nini anamtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa jina la uhuru wa maoni?
-
Kiongozi Muadhamu aushangaa undumakuwili wa Rais Macron wa Ufaransa
Oct 29, 2020 03:57Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kushangazwa kwake na undumakuwili wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kulikingia kifua jarida la Charlie Hebdo la nchini hiyo ya Ulaya kwa kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.
-
Maandamano ya kulaani misimamo ya Macron dhidi ya Uislamu yafanyika Iran na Iraq
Oct 29, 2020 03:23Maelfu ya Waislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq wamefanya maandamano ya kulaani hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuunga mkono vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW na matukufu ya Kiislamu.
-
EuroMed Rights yakosoa chuki na uhasama Wa viongozi wa Ufaransa dhidi ya Waislamu
Oct 28, 2020 23:25Kituo cha Haki za Binadamu Ulaya na Mediterania (EuroMed Rights) kimeItaja hatua ya viongozi wa Ufaransa ya kueneza chuki na uhasama dhidi ya Waislamu kuwa ni hatari kubwa.
-
Ayatullah Larijani ataka Waislamu waungane kukabili chuki dhidi yao
Oct 28, 2020 04:22Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Iran amelaani vikali hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuunga mkono kitendo cha kifidhuli cha jarida la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa Waislamu kuwa na umoja na ushirikiano katika kukabiliana na chuki dhidi yao na Uislamu.
-
Radiamali ya kindumakuwili ya Ufaransa kufuatia malalamiko ya Waislamu duniani
Oct 28, 2020 04:11Waislamu duniani kote wamekasirishwa na kushadidi vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa hasa cha kuchapishwa tena katuni zinazomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW. Hasira za Waislamu zimeongezeka maradufu baada ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutetea vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu kwa kisingizo cha uhuru wa maoni.
-
Maelfu waandamana Bangladesh wakitaka kususiwa bidhaa za Ufaransa
Oct 28, 2020 01:01Makumi ya maelfu ya Waislamu wa Bangladesh wamefanya maandamano katika mji mkuu Dhaka, kulaani hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuunga mkono kitendo cha kifidhuli cha jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
-
Mufti wa Oman: Waislamu waondoe mitaji yao katika sekta za uchumi za Ufaransa
Oct 27, 2020 03:55Mufti wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili amewatolea mwito Waislamu wa kuondoa mitaji yao waliyowekeza kwenye vituo na sekta za uchumi za Ufaransa.
-
Erdogan: Bidhaa za Ufaransa zisusiwe... viongozi wa sasa wa Ulaya ni Manazi na Mafashisti
Oct 27, 2020 03:54Wakati mtifuano wa kisiasa baina ya Ufaransa na Uturuki ukiwa unaendelea baada ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kutoa matamshi ya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu na Waislamu, Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki ametoa mwito wa kususiwa bidhaa za Ufaransa.