-
Kwa nini utawala wa Kizayuni hauna uwezo wa kukabiliana na mashambulizi ya makombora ya muqawama wa Yemen?
Aug 27, 2025 22:56Maafisa wa utawala wa Kizayuni wamekiri kwamba utawala huo hauna uwezo wa kukabiliana na mashambulizi ya makombora ya muqawama wa Yemen, ambayo yanalenga kwa usahihi mkubwa shabaha zilizoko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
Je, inatosha kwa nchi za Magharibi kulaani kwa maneno matupu jinai za utawala wa Israel?
Aug 25, 2025 23:12Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 21 za Magharibi kwa pamoja wamelaani uamuzi wa Israel wa kujenga makaazi mapya ya walowezi wa Kizayuni huko Quds Mashariki.
-
Tangu Agosti 6, jeshi la Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 ya Mji wa Ghaza
Aug 25, 2025 03:29Shirika la Ulinzi wa Raia la Palestina limetangaza kuwa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 katika vitongoji vya Zeitoun na Sabra katika Mji wa Ghaza tangu lilipoanza kuuvamia mji huo mnamo Agosti 6, na hivyo kupelekea mamia ya Wapalestina kunasa chini ya vifusi vya majengo hayo.
-
EU yasisitiza kuiunga mkono "kwa dhati" ICC baada ya US kuwawekea vikwazo waendesha mashtaka 2
Aug 25, 2025 03:08Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema "amesikitishwa sana" na uamuzi wa Marekani wa kuwawekea vikwazo maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
Ufaransa 'yamjia juu' balozi wa US Paris kwa kuituhumu kuwa inahatarisha maisha ya Mayahudi
Aug 25, 2025 03:08Ufaransa imemwita balozi wa Marekani nchini humo Charles Kushner, baada ya mwanadiplomasia huyo kumwandikia barua Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akidai kwamba Paris imeshindwa kuchukua hatua za kutosha kukomesha vitendo vya mabavu dhidi ya Mayahudi raia wa nchi hiyo.
-
Imefichuka kupitia taarifa za siri za jeshi la Israel: 83% ya waliouawa Ghaza ni raia wa kawaida
Aug 22, 2025 06:34Taarifa za siri za jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel zilizovuja zinaonyesha kuwa watu watano kati ya sita waliouliwa na jeshi hilo katika Ukanda wa Ghaza ni raia wa kawaida.
-
Raia 102 wa kigeni magaidi na matapeli wa mitandaoni watimuliwa Nigeria, wengi wao ni Wachina
Aug 22, 2025 06:34Serikali ya Nigeria imewatimua raia wa kigeni 102 wakiwemo Wachina 50 waliopatikana na hatia ya kuhusika na "ugaidi wa mitandaoni na utapeli wa mitandaoni".
-
Jibu la Tunisia kwa kauli ya Netanyahu ni ishara ya wasiwasi wa nchi za Kiarabu kuhusu mipango ya upanuzi ya Israel
Aug 21, 2025 22:43Wananchi wa Tunisia wamefanya maandamano ya kupinga uzayuni wakilaani matamshi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, kuhusu kile kinachoitwa “Israeli Kubwa.”
-
Familia za mateka Waisrael zaanzisha mgomo wa nchi nzima kupinga upanuzi wa vita dhidi ya Ghaza
Aug 17, 2025 23:24Gazeti la Times of Israel limeripoti kuwa familia na waungaji mkono wa mateka Waisrael wameanza mgomo wao wa nchi nzima ili "kupinga upanuzi wa vita katika Ukanda wa Ghaza badala ya kusaini makubaliano ya kufanikisha kuachiliwa huru mateka hao wanaoshikiliwa na Hamas".
-
UN: Israel imeshaua Wapalestina wasiopungua 1,760 Ghaza wanaokimbilia msaada wa chakula
Aug 16, 2025 03:09Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa tangu mwishoni mwa mwezi Mei hadi sasa, jeshi la Israel limeshawaua Wapalestina wasiopungua 1,760 walipokuwa wakihangaika kupata msaada wa chakula huko Ukanda wa Ghaza likiwa ni ongezeko la mamia kadhaa tangu ilipotoa takwimu zake za mwisho mwanzoni mwa mwezi huu wa Agosti.