-
Wafungwa wa Misri wasusia chakula kukosoa 'kesi bandia'
May 23, 2016 07:47Makumi ya wafungwa wa Misri walioshiriki maandamano ya kuikosoa serikali ya Cairo kwa kuipa Saudi Arabia visiwa viwili vinavyomilikiwa na nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika wanafanya mgomo wa kula, kulalamikia kile walichokitaja kuwa kesi bandia na za kidhulma dhidi yao.