Pars Today
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO amesisitiza kuwa mji mtakatifu wa Quds ni mstari mwekundu kwa Wapalestina, kwa ulimwengu wa Kiarabu, kwa Waislamu na pia kwa Wakristo ulimwenguni.
Shirika la habari la Ufaransa AFP limetangaza kuwa, wafuasi wa dini za wachache wakiwemo Wakristo wanaishi kwa usalama mkubwa nchini Iran na kwamba nchi hiyo ni katika nchi zenye usalama mkubwa zaidi kwa watu wa dini za wachache kwenye eneo la Mashariki ya Kati.
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa salamu za kheri na fanaka kwa viongozi wa nchi za Wakristo duniani kwa mnasaba wa kuwadia Krismami, siku ya kukumbuka kuzaliwa Nabii Issa Masih AS (Yesu).
Jamii ya wanasheria nchini Ireland, imewawajibisha mawakili na washauri wa sheria Waislamu kutumia Qur'ani Tukufu wakati wa kula kiapo.
Mhubiri Mkristo wa Marekani amehukumiwa miaka 40 jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto katika kituo kimoja cha mayatima chini Kenya.
Waislamu na Wakristo wa Cameroon wanaandaa mikakati ya kupambana na kundi la Boko Haram la nchini Nigeria.