• Malengo na mbinu za Wamagharibi katika kueneza chuki dhidi ya Iran na Uislamu

    Malengo na mbinu za Wamagharibi katika kueneza chuki dhidi ya Iran na Uislamu

    Apr 20, 2016 06:03

    Baada ya kusambaratika mfumo wa ncha mbili wa kambi za Magharibi na Mashariki, jumuiya ya kimataifa ingali katika kipindi cha mpito. Katika kipindi hiki cha mpito, nchi za Magharibi zinazodai kuwa na utamaduni bora zinadai kuwa kufuatia kusambaratika mfumo wa Kikomunisti, hakuna tena chaguo jngine isipokuwa Demokrasia ya Kiliberali katika dunia.