-
Sababu na taathira za mauaji ya kigaidi ya kamanda Qassem Soleimani kwa mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah
Jan 06, 2020 11:12Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amebainisha sababu, matokeo na taathira za jinai iliyofanywa na Marekani, ya kumuua kigaidi kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq Abu Mahdi Al-Muhandis pamoja na wanamuqawama wengine kadhaa; na akasisitiza kwamba, jinai hiyo ya Washington itapelekea kuanza historia mpya Asia Magharibi.
-
Kiongozi Muadhamu asalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Soleimani na mashahidi wenzake + Video
Jan 06, 2020 08:16Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi amesalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na mashahidi wenzake waliouliwa kigaidi na Marekani nchini Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020.
-
Rouhani: Inabidi tusimame imara katika kukabiliana na uingiliaji wa Marekani
Jan 06, 2020 08:15Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, usiku wa kuamkia leo amefanya mazungumzo ya simu na Rais Barham Salih wa Iraq na kusisitiza kuwa, ni jambo zito mno kwa mataifa makubwa ya Iran na Iraq kuweza kuvumilia mauaji ya kigaidi waliyofanyiwa Alhaj Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wanamapambano wenzao waliokuwa wamefuatana nao.
-
Hatua ya kwanza nchini Iraq, mwanzo wa historia mpya magharibi mwa Asia
Jan 06, 2020 08:15Bunge la Iraq jana lilipasisha muswada wa kuwafukuza askari wa Marekani nchini humo. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wito uliotolewa na wananchi, wanasiasa na makundi mbalimbali ya Iraq baada ya jeshi la Marekani kumuua kigaidi Jemedari Qassem Solaimani na naibu kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes.
-
Iran: Marekani ikitushambulia tutaingamiza Israel na kuifuta katika uso wa dunia
Jan 06, 2020 08:14Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika maombolezo ya kukumbuka kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani; Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kwamba, iwapo Marekani itatekeleza vitisho vinavyotolewa na Trump vya kuishambulia Iran, basi wawe na yakini kwamba miji ya Haifa na Tel Aviv na maeneo mengine muhimu ya Israel yataangamizwa kikamilifu na kusawazisha na ardhi.
-
Waziri Mkuu wa Iraq: Soleimani alikuwa mgeni wangu rasmi aliyekuja na ujumbe wa Saudi Arabia
Jan 06, 2020 08:13Kaimu Waziri Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi amesema kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alielekea nchini Iraq akiwa mgeni rasmi wa serikali na alikwenda na ujumbe wa Saudi Arabia kuhusu mazungumzo.
-
Ismail Hania ametoka Ghaza kuja Tehran kushiriki maziko ya Kamanda Soleimani; asema Soleimani ni shahidi wa Quds + Video
Jan 06, 2020 08:13Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.
-
Kiongozi wa Russia: Jenerali Qassem Soleimani alikuwa shujaa wa ulimwengu wote wa Kiislamu
Jan 06, 2020 02:45Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa inayoitwa 'Umma Mmoja wa Kiislamu' nchini Russia amesema kuwa, Meja Jenerali Qassem Soleimani, hakuwa tu mtu wa Iran, Iraq au Syria, bali ni shakhsia wa Kiislamu na ulimwengu kwa ujumla.
-
Vitisho vipya vya Trump kutokana na wahka wa ulipizaji kisasi wa Iran
Jan 06, 2020 02:43Hatua ya kijinai na iliyo kinyume cha sheria ya Marekani ya kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq pamoja na shakhsia wengine huko mjini Baghdad, imekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa Iran ambayo imesisitizia kulipiza kisasi kikali kwa Marekani.
-
Muqtada al-Sadr: Ubalozi na kambi zote za kijeshi za Marekani nchini Iraq zipigwe kufuli mara moja
Jan 05, 2020 16:26Muqtada al-Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ametoa ujumbe leo kwenda kwa spika wa bunge akitaka kupigwa kufuli ubalozi wa Marekani na kambi zake za kijeshi nchini humo.