Pars Today
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanyia majaribio kwa mafanikio kombora lake jipya la majini kwa ardhi kwa kutumia nyambizi yake aina ya Ghadir.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi Ayatullah Sayyed Ali Khamenei leo amekutana na makamanda na wakuu wa jeshi la wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi la Wanamaji.
Kamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeri Hossein Khanzadi amesema kuleta amani katika eneo na kwenye maji huru ya kimataifa ni miongoni mwa malengo muhimu zaidi na majukumu ya jeshi hilo.
Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema tarehe 7 Azar (28 Novemba) ambayo ni siku ya Jeshi la Majini ni siku ya fahari na heshima, na siku ya kuenzi kujitolea mhanga kwa jeshi hilo.
Meli za Kivita za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimesindikiza zaidi ya meli 4,200 za kibiashara katika eneo linalosumbuliwa na maharamia la Ghuba ya Aden tokea mwaka 2008.
Maharamu kutoka Somalia waliojaribu kuteka nyara meli ya mizigo ya Iran wametimuliwa na manwoari za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.