Feb 22, 2016 03:35
Mwakilishi wa Jumuiya ya Mayahudi wa Isfahan magharibi mwa Iran amesema kuwa, kupewa nafasi wafuasi wa dini zote za tawhidi katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ni katika sifa za kipekee za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.