-
Bara la Afrika laongoza katika mauaji ya wanawake duniani
Nov 26, 2024 09:47Imebainika kuwa wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa watu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja aliuawa katika kila dakika 10, na kwa mantiki hiyo ni jumla ya wanawake 85,000 waliouawa huku bara la Afrika likiongoza.
-
Magenge yenye silaha yauwa watu 30 katika muda wa siku 3 huko Benue, Nigeria
Nov 25, 2024 23:24Watu wasiopungua 30 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya magenge yenye silaha yaliyojiri kwa muda wa siku tatu dhidi ya wakulima jamii mbalimbali katika jimbo la Benue kaskazini kati nchini Nigeria.
-
Umoja wa Mataifa unatafuta ufadhili zaidi kwa misaada ya kibinadamu nchini Sudan
Nov 25, 2024 22:56Shirika rasmi la habari la Sudan SUNA limeripoti kuwa, Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali ya nchi hiyo kutafuta wafadhili wa mipango yake ya misaada ya kibinadamu kwa ajaili ya mwaka ujao wa 2025.
-
UN yaitaka Somalia iongeze uwekezaji katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia
Nov 25, 2024 22:55Umoja wa Mataifa jana Jumatatu ulitoa mwito kwa serikali ya Somalia kuongeza uwekezaji katika vita dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia nchini humo.
-
Watu 45 hawajulikani walipo baada ya boti kuzama nchini Misri
Nov 25, 2024 22:55Takriban watu 45, wakiwemo watalii 31 na wafanyakazi 14 wametoweka baada ya boti yao kuzama katika eneo la kaskazini mwa mji wa Marsa Alam wa Bahari Nyekundu kwenye mkoa wa Bahari Nyekundu nchni Misri.
-
Wananchi wa Malawi waandamana kulalamikia uhaba mkubwa wa petroli na dizeli
Nov 25, 2024 10:01Polisi katika mji wa Lilongwe nchini Malawi leo Jumatatu wametumia gesi ya kutoa machozi kutawanya umati wa waandamanaji waliotaka kujiuzulu Waziri wa Nishati na Madini wa nchi hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta ya petroli na dizeli katika miji mbalimbali ya nchi hiyo unaoendelea kwa muda wa mwezi mmoja sasa.
-
Naibu rais aliyetimuliwa Kenya aishambulia serikali ya Rais Ruto, asema haisikilizi vilio vya watu
Nov 25, 2024 04:33Naibu Rais wa Kenya aliyeng'olewa madarakani, Rigathi Gachagua, ameishambulia serikari ya bosi wake wa zamani, Rais William Ruto, akisema imeziba masikio kwa vilio vya watu walioichagua akisisitiza kwamba hatimaye ataondolewa lawama zote "alizobambikiziwa" alipoondolewa mamlakani.
-
Wakili Lukwago: Kenya ilihusika kukamatwa Kizza Besigye
Nov 25, 2024 00:02Wakili wa kiongozi wa upinzani nchini Uganda amesema kuwa, inaonekana mamlaka za Kenya zilihusika pakubwa katika kukamatwa huko Nairobi Kizza Besigye na kumuondoa nchini kinyume cha sheria.
-
Kiongozi maarufu wa upinzani Tanzania na wenzake waachiliwa huru kwa dhamana
Nov 24, 2024 03:57Freeman Mbowe, kiongozi wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania jana aliachiliwa huru kwa dhamana baada ya kukamatwa siku ya Ijumaa yaani siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Novemba 27 nchini humo.
-
Uhusiano wa Niger na nchi za Ulaya wazidi kuharibika, EU yamwita balozi wake
Nov 24, 2024 03:55Umoja wa Ulaya (EU) umemuondoa balozi wake aliyekuweko Niamey, mji mkuu wa Niger kutokana na kushadidi mvutano na uongozi mpya wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Serikali ya Niger inalalamika kwamba nchi za Ulaya zinataka kuidhibiti nchi hiyo kupitia misaada ya kibinadamu.