-
Mshindi wa Tuzo ya Nobel, Denis Mukwege: Makubaliano ya amani kati ya Kinshasa na M23 ni 'haramu'
Dec 02, 2025 02:53Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Dkt. Denis Mukwege amelaani mchakato wa amani unaoendelea kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 unaolenga kukomesha mapigano mashariki mwa DRC.
-
UN yatahadharisha kuhusu janga la njaa linalotishia wakimbizi nchini Ethiopia
Dec 01, 2025 23:12Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa (WFP) limeonya kwamba wakimbizi nchini Ethiopia wako katika hatari ya kufa njaa kutokana na uhaba mkubwa wa fedha unaolilazimisha shirika hilo kupunguza mgao wa chakula.
-
Cameroon: Mpinzani wa Rais Biya amefariki dunia akiwa kizuizini
Dec 01, 2025 11:13Kiongozi wa kisiasa na kinara wa chama cha upinzani cha Manidem nchini Cameroon, Anicet Ekane, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Desemba 1.
-
Ethiopia yazindua mkakati wa miaka mitano wa kuendeleza uchumi wa kidijitali
Dec 01, 2025 06:55Serikali ya Ethiopia imezindua Mkakati wa Kidijitali wa Ethiopia 2030, unaolenga kukuza matumizi ya teknolojia katika sekta zote za kiuchumi na kuugeuza uchumi wa nchi hiyo ya Pembe ya kuwa wa kidijitali kikamilifu.
-
Baraza la Uongozi la Sudan lasisitiza kuwa liko tayari kushirikiana na UN
Dec 01, 2025 06:55Mkuu wa Baraza Kuu la Mpito la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono juhudi za kibinadamu, maendeleo na jitihada za kijamii za nchi hiyo.
-
Wabeba silaha wateka nyara watu wengine 14 Nigeria, yumo bibi harusi na kitoto kichanga
Dec 01, 2025 02:14Washambuliaji wenye silaha wamewateka nyara wanawake 13 na mtoto mchanga katika hujuma mpya ya uvamizi uliofanywa usiku wa kuamkia jana Jumapili kaskazini mashariki mwa Nigeria, ukiwa ni mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni ya utekaji nyara mkubwa unaoshuhudiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
-
Rais wa Afrika Kusini amtuhumu Trump kwa kutoa 'kauli zisizo za kweli' kuhusu nchi yake
Nov 30, 2025 23:37Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alimtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuendelea kutoa "taarifa zisizo za kweli" kuhusu nchi yake.
-
Ushahidi wa kwanza: Gesi ya klorini imetumika katika vita vya ndani Sudan
Nov 30, 2025 08:57Uchunguzi wa timu ya FRANCE 24 Observers unaonyesha namna gesi ya klorini ilivyotumika kama silaha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Sudan.
-
Marais wa Rwanda na DRC kutia saini makubaliano ya amani
Nov 30, 2025 04:11Marais Felix Tshisekedi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wiki ijayo wanatarajiwa kutia kusaini makubaliano ya mwisho yanayolenga kufikia amani ya kudumu mashariki mwa Congo.
-
Spika wa bunge la Libya atoa mwito wa kufanyika uchaguzi wa haraka wa rais
Nov 29, 2025 23:06Spika wa Bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo ametoa mwito kwa Tume Kuu ya Uchaguzi kutekeleza mara moja sheria ya kuitisha haraka uchaguzi wa rais wa moja kwa moja.