-
Kampeni za uchaguzi mkuu wa Uganda wa Januari 2026 zaanza rasmi
Sep 29, 2025 08:03Kampeni za uchaguzi mkuu wa Uganda zimeanza rasmi leo Jumatatu kabla ya uchaguzi huo wa Januari 206 ambao huenda ukawa mpambano kati ya Rais aliyeko madarakani Yoweri Kaguta Museveni na mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi Ssentamu, almaarufu Bobi Wine, ukitazamwa kama marudio ya uchaguzi wa 2021.
-
Watu 95 wafariki dunia kwa njaa na magonjwa Sudan
Sep 29, 2025 03:06Watu 95 wamefariki dunia kutokana na njaa pamoja na magonjwa katika kipindi cha siku 40 zilizopita kwenye kambi ya wakimbizi ya Abu Shouk huko El Fasher nchini Sudan. Hayo yameelezwa na wafanyakazi wa kujitolea.
-
Jeshi la Sudan latangaza kupata ushindi mkubwa, RSF wakanusha
Sep 28, 2025 22:47Jeshi la Sudan (SAF) limetangazaa kuwa limepata ushindi mkubwa katika mapambano yake na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika eneo la Kordofan, huko Magharibi mwa Sudan. Hata hivyo RSF wamekanusha madai hayo.
-
Uchaguzi wa rais wa Ushelisheli waingia duru ya pili
Sep 28, 2025 07:32Tume ya Uchaguzi ya Ushelisheli imetangaza leo Jumapili kwamba, uchaguzi wa rrais uliofanyika hivi karibuni utaingia duru ya pili, kwani hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura katika duru ya kwanza.
-
Niger katika Mkutano wa UNGA: Ufaransa inapasa kukumbuka na kutambua jinai zake
Sep 28, 2025 03:32Lamine Zeine Ali Mahaman Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Niger ameikosoa Ufaransa nchi mkoloni wa zamani wa nchi hiyo akisema kuwa nchi hiyo ya Ulaya inatumia ugaidi kudhoofisha taifa hilo la eneo la Sahel.
-
Maelfu waandamana Afrika Kusini wakitaka kukatwa uhusiano wa nchi hiyo na Israel
Sep 28, 2025 03:31Watu zaidi ya elfu tatu jana waliandamana katika mji wa Cape Town Afrika Kusini wakiitaka nchi hiyo kukata uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na Israel, ikiwa ni pamoja na kufunga ubalozi wake kufuatia vita na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
-
Watu 100 wahofiwa kuaga dunia kwa kufukiwa mgodini Nigeria
Sep 27, 2025 22:59Takribani watu 100 wanahofiwa kufariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi vya mgodi wa dhahabu katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Zaidi ya raia 100 watekwa nyara Ituri na wanamgambo wa CODECO
Sep 27, 2025 22:57Raia zaidi ya 100 wametekwa nyara katika mkoa wa Ituri katika shambulio la wanamgambo wa Codeco. Raia waliotekwa nyara walikuwa wakirejea kutoka soko la Bule.
-
Rais wa Madagascar alaani uporaji, atoa mwito wa utulivu
Sep 27, 2025 06:53Rais Andry Rajoelina wa Madagascar amelaani matukio ya vurugu yaliyotokea hasa katika mji mkuu Antananarivo na kuwataka wananchi wote wa Madagascar kuwa watulivu.
-
Rais wa Afrika Kusini ataka kushughulikiwa changamoto za kiuchumi duniani
Sep 27, 2025 06:51Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mwito kwa taasisi za kimataifa kufanya mageuzi ya maana ambayo yatashughulikia changamoto zinazoukabili uchumi wa dunia.