-
Pezeshkian:Uhusiano wa Iran na Armenia haupaswi kuvurugwa na dola la kigeni
Aug 31, 2025 01:06Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa Iran na Armenia hazipaswi kuruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuvuruga uhusiano wao wa kirafiki na wa kimkakati.
-
Larijani: Iran inapinga mabadiliko ya kijiografia katika ukanda wa Kavkazia
Aug 31, 2025 01:06Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Larijani, ameeleza kuwa Tehran inapinga vikali hatua yoyote inayoweza kuathiri muundo wa kisiasa na kijiografia wa eneo la Kavkazi (Caucasus)
-
Iran yawakamata majasusi wa Mossad waliohusika katika vita
Aug 31, 2025 01:05Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) kimetangaza kukamatwa kwa mtandao wa kigaidi unaohusishwa na shirika la ujasusi la Israel, Mossad, katika mkoa wa Khorasan Razavi. Majasusi hao walihusika katika shughuli za ujasusi na hujuma ndani ya Iran wakati wa mashambulizi ya siku 12 yaliyofanywa na Israel dhidi ya taifa hilo.
-
Iravani: Iran haitafanya mazungumzo kwa vitisho au kwa kushurutishwa
Aug 30, 2025 09:33Amir-Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, ameitaja hatua ya nchi tatu za Ulaya yaani Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ya kuanzisha kuanzisha mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran (snapback) hatua 'isiyo ya kisheria', na kuongeza kuwa hatua hiyo inapuuza Utaratibu wa Utatuzi wa Mizozo (DRM) wa makubaliano9 ya nyuklia ya JCPOA.
-
Pezeshkian: Iran iko tayari kutumia misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa mafuriko Pakistan
Aug 30, 2025 08:56Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi na kutoa mkono wa pole kwa serikali ya wananchi wa Pakistan kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu wengi na kuharibiwa mali. Amesema Iran iko tayari kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko nchini Pakistan.
-
Sababu za Iran kuitambua hatua ya Troika ya Ulaya ya kutekeleza snapback kuwa kinyume cha sheria
Aug 30, 2025 07:16Kikao cha faragha cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushughulikia uzinduzi wa mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kurejesha vikwazo vya Baraza la Usalama dhidi ya Iran (snapback) wa Troika ya Ulaya kilifanyika jana Ijumaa, Agosti 29.
-
Iran: Ulaya haina mamlaka ya kisheria ya kuanzisha vikwazo upya
Aug 29, 2025 07:39Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amepinga vikali juhudi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani (E3) za kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyofutwa chini ya Azimio 2231 la mwaka 2015, akitaja hatua hiyo kuwa “batili na isiyo na athari.”
-
Haj Ali Akbari: Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ni watumishi wa Wazayuni
Aug 29, 2025 07:33Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amekosoa vikali hatua ya hivi karibuni ya mataifa matatu ya Ulaya dhidi ya Iran, akiitaja kuwa ni haramu, ya kisiasa na iliyotekelezwa kwa mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran yamesababisha Israel hasara ya mabilioni
Aug 29, 2025 07:13Maafisa wa utawala wa Israel wamethibitisha kuwa mashambulizi ya kisasi ya Iran dhidi ya taasisi za Israel wakati wa vita vya siku 12 yamesababisha hasara ya mabilioni ya shekel kwa utawala huo, huku zaidi ya madai 53,599 ya fidia yakiwasilishwa.
-
Russia na China zasimama na Iran dhidi ya E3 kwa kutumia vibaya azimio la UN
Aug 29, 2025 04:08Russia na China zimechukua hatua kukabiliana na mpango wa nchi tatu zinazounda Troika ya Ulaya, E3, na kusambaza rasimu ya azimio katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalopendekeza "urefushaji wa kiufundi" kwa muda wa miezi sita utekelezaji wa Azimio 2231 la baraza hilo.