-
Rais Pezeshkian asisitizia haja ya kuimarisha uhusiano wa Iran na Madagascar
Aug 28, 2025 23:46Rais Masoud Pezeshkian amewataka mabalozi wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu katika nchi za Madagascar na Croatia kuimarisha uhusiano wa pande mbili baina ya Iran na nchi hizi mbili.
-
Iran yalaani vikali hatua ya E3 kutekeleza "snapback", yasema haina uhalali kisheria
Aug 28, 2025 23:46Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali uamuzi uliochukuliwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza siku ya Alkhamisi wa kuanzisha utaratibu wa "snapback" wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kurejesha papo kwa papo vikwazo vya baraza hilo dhidi yake kutokana na mpango wake wa nyuklia.
-
Iran ilishinda vita dhidi ya Israel na Marekani, ilimlazimisha adui akubali kushindwa
Aug 28, 2025 08:23Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ilishinda katika vita vya siku 12 vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Israel mwezi Juni, na ilifanikiwa kumlazimisha aduia akubali kushindwa.
-
Iran yaionya E3: Fanyeni chaguo la busara, mkitekeleza 'snapback' ushirikiano na IAEA utasita
Aug 28, 2025 03:41Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezionya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwamba itasitisha maingiliano yake na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya nyuklia iwapo nchi hizo tatu zitalifanya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lirejeshe vikwazo dhidi yake.
-
Waziri wa Ulinzi: Vikosi vya Iran vilipenya mifumo ya ulinzi wa makombora ya Israel
Aug 28, 2025 00:49Waziri wa Ulinzi wa Iran amesifu uwezo wa hali ya juu wa kijeshi wa taifa hili wakati wa vita vya siku 12 vya uchokozi vilivyoanzishwa na Marekani na Israel, akisema kuwa Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viliweza kupenya mifumo ya ulinzi yenye tabaka nyingi ya utawala wa kichokozi wa Israel na kusambaratisha ngome kadhaa za kijeshi kwa kutumia makombora ya kisasa.
-
Iran yakosoa uamuzi wa Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa nchi hizi mbili
Aug 28, 2025 00:48Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechapisha taarifa ikiutaja uamuzi wa serikali ya Australia wa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia na Iran kuwa kinyume na utamaduni wa uhusiano mkongwe wa nchi hizi mbili.
-
Araqchi: Kufunga Mlango Bahari wa Hormuz si sera rasmi ya Iran
Aug 27, 2025 07:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesisitiza kuwa suala la kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz si msimamo rasmi wa Iran, na kusisitiza kuwa sera ya Tehran ni kudumisha amani na utulivu katika Ghuba ya Uajemi.
-
Polisi ya Iran yaangamiza magaidi 8 waliohusika na shambulizi la kigaidi Sistan na Baluchestan
Aug 27, 2025 07:16Polisi ya Iran imetoa kipigo kikubwa kwa magaidi wanaoungwa mkono na nchi ajinabi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini-mashariki mwa Iran, kwa kuwaangamiza magaidi 8 waliohusika na shambulio baya la karibuni dhidi ya maafisa wa polisi katika mkoa huo.
-
Kwa nini Iran inataka hatua kali zaidi zichukuliwe na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu dhidi ya utawala wa Kizayuni?
Aug 27, 2025 03:44Seyyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran karibuni hivi alifika mjini Jeddah, Saudia kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha dharura cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na kukitaja kikao hicho kuwa mtihani wa kihistoria kwa Umma wa Kiislamu na pengine miongoni mwa fursa chache za kuunda muungano wa kieneo na kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Araqchi: Hatua ya Australia ya kumfukuza balozi wa Iran ni kutaka kuiridhisha Israel
Aug 27, 2025 03:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani uamuzi wa Australia wa kumfukuza balozi wa Tehran nchini humo kutokana na madai eti ya mashambulizi kwenye vituo vya Kiyahudi, na kueleza kuwa ni kitendo cha kutaka kuiridhisha "serikali inayoongozwa na wahalifu wa kivita."