-
Iran yaapa kulipiza kisasi baada ya Australia kumfukuza balozi wake
Aug 26, 2025 11:43Iran imeapa kuchukua hatua zinazofaa za kulipiza kisasi baada ya Australia kumfukuza balozi wa Jamhuri ya Kiislamu nchini humo kwa madai ya "chuki dhidi ya Wayahudi," na kusisitiza kwamba vitendo vya ubaguzi wa kidini havina nafasi katika utamaduni, historia au imani ya taifa la Iran.
-
Iran yakanusha madai ya Trump kuhusu kutengeneza silaha za nyuklia
Aug 26, 2025 02:34Iran imekanusha tuhuma zilizotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa amani wa taifa hili, ikisema madai hayo yametegemea kauli zilizopitwa na wakati ambazo zilitolewa na raia wa kawaida wa Iran.
-
Pezeshkian amwambia Putin: Iran haijawahi kamwe kutaka kumiliki silaha za nyuklia
Aug 26, 2025 00:12Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Jumatatu alizungumza kwa simu na Rais Vladimir Putin wa Russiai na kumweleza kuwa Tehran haijawahi kutaka kumiliki wala haitatafuta silaha za nyuklia, akisisitiza msimamo wa muda mrefu wa Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.
-
Araghchi: Historia haitasamehe usuasuaji zaidi katika kukomesha janga la Gaza
Aug 25, 2025 08:20Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kimataifa kukomesha mauaji ya halaiki ya Israel yanayoendelea huko Gaza, akisema kuwa nchi zote zinapaswa kusimama upande sahihi wa historia ambao "hautasamehe" ucheleweshaji wowote zaidi wa kupunguza mateso ya watu wa Palestina.
-
Pezeshkian: Migawanyiko kati ya mataifa ya Kiislamu inainufaisha Israel pekee
Aug 25, 2025 07:30Rais wa Iran amesema umoja wa wananchi wa Iran na katika mataifa yote ya Kiislamu ndiyo kinga kuu dhidi ya vitisho vya maadui, akionya kuwa migawanyiko ni kwa maslahi ya Israel pekee.
-
Iran na Ulaya kuendelea na mazungumzo ya nyuklia mjini Geneva
Aug 25, 2025 07:03Iran na nchi tatu zenye nguvu za Ulaya - Ujerumani, Ufaransa na Uingereza - zinatazamiwa kuanza tena mazungumzo ya nyuklia huko Geneva, Uswisi siku ya Jumanne, yakiangazia maswala ya nyuklia na uondoaji wa vikwazo.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran itasimama kidete dhidi ya matakwa ya Marekani
Aug 24, 2025 09:35Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Marekani inahujumu na kukabiliana na Iran kwa sababu inataka taifa hili liwe tiifu kwake, lakini wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu watapambana vikali na “tusi hilo kubwa”.
-
Araqchi atahadharisha kuhusu njozi za "Israel Kubwa" kabla ya mkutano wa dharura wa OIC
Aug 24, 2025 08:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ametahadharisha kuwa kuwepo njozi za "Israel Kubwa" kunawakilisha hatari na tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia. Araqchi amezitolea wito nchi za Kiislamu kuchukua hatua za pamoja kukabiliana na ajenda ya kujitanua ya Israel.
-
IRGC: Uhusiano wa kina kati ya serikali, wananchi na vikosi vya ulinzi ni dhamana ya Iran yenye nguvu
Aug 24, 2025 07:25Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeashiria umuhimu wa uhusiano wa kina uliopo kati ya serikali, taifa na vikosi vya ulinzi likiutaja kuwa muhimu kwa ajili ya kuwa na nchi yenye nguvu na iliyoendelea. Jeshi la IRGC aidha limesisitiza dhamira yake ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi na usalama kwa kuzingatia vitisho vilivyopo.
-
Rais Pezeshkian aipongeza timu ya astronomia ya Iran kwa kushinda ubingwa wa dunia
Aug 24, 2025 04:34Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameipongeza Timu ya Olimpiadi ya Astronomia ya Iran kwa kushinda taji la ubingwa wa dunia kwa mwaka wa pili mfululizo.