-
Imam wa Swala ya Ijumaa Tehran: Vita vya Siku 12 vilikuwa dhihirisho la imani ya Tauhidi ya taifa la Iran
Jul 04, 2025 11:57Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema: "Mienendo na matua za wananchi wa Iran katika vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel vilikuwa dhihirisho la Tauhidi."
-
Iran: Marekani ithibitishe dhamira yake ya diplomasia kabla ya kuanza tena mazungumzo ya nyuklia
Jul 04, 2025 03:44Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema, Tehran haitashiriki tena mazungumzo ya nyuklia isipokuwa pale Marekani itakapoonyesha dhamira ya kweli ya diplomasia na kuacha kuitumia kama chombo cha mashinikizo au udanganyifu.
-
Araqchi: Ujerumani imeonyesha uadui wake kwa kuunga mkono mashambulizi dhidi ya Iran
Jul 04, 2025 00:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi amejibu maandishi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani katika mtandao wa kijamii wa X kuhusu uamuzi wa Iran wa kusitisha ushirikiano wake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki baada ya Israel na Marekani kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran.
-
Araqchi: Mazungumzo ya kuhitimisha mpango wa nyuklia wa Iran hayakubaliki
Jul 03, 2025 10:59Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza kuwa, ikiwa lengo la mazungumzo ni kuhitimisha mpango wa nyuklia wa Iran, jukumu na ushiriki wa Ulaya na Uingereza katika mchakato wa mazungumzo hayo litakuwa batili na hilo halina maana yoyote.
-
Utafiti: Asilimia 77 ya Wairani 'wanajivunia' uwezo wa makombora na droni wa jeshi dhidi ya uvamizi wa Israel
Jul 03, 2025 04:13Wairani wasiopungua asilimia 77 wameeleza kuwa wanahisi kuwa na fakhari kubwa kufuatia jibu lililotolewa na vikosi vya ulinzi mkabala wa uvamizi wa Israel dhidi ya Iran. Takwimu hii ni kwa mujibu wa utafiti ulioendeshwa na Kitengo cha Utafiti cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).
-
Makamanda wa juu waahidi kutoa kipigo kikali zaidi iwapo Iran itashambuliwa tena
Jul 03, 2025 04:08Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Iran amewaonya maadui kwamba watapata kipigo kikali zaidi iwapo wataanzisha uchokozi mpya dhidi ya Iran.
-
Araqchi: Vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kukabiliana na uchokozi wowote wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake
Jul 03, 2025 04:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya Iran viko tayari kabisa kukabiliana kwa nguvu zake zote na chokochoko za aina yoyote za utawala wa Kizayuni na pande zinazouunga mkono utawala huo.
-
Iran yakataa takwa la EU la kujadili kusitisha mpango wake wa nyuklia
Jul 03, 2025 01:09Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepinga msimamo wa Umoja wa Ulaya (EU) wa hivi karibuni unaotaka kuanzishwa mazungumzo mapya yenye lengo la kusitisha mpango wa nyuklia wa Iran.
-
UNESCO yaionya Israel kuhusu kulenga kijeshi maeneo ya urithi wa kihistoria ya Iran
Jul 02, 2025 08:34Waziri wa Turathi za Kitamaduni, Utalii na Sanaa za Mikono wa Iran amesema kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ametoa onyo kwa Israel na kuutaka utawala huo kutojaribu kulenga maeneo ya turathi za kihistoria na kitamaduni ya Iran.
-
Rais wa Iran aidhinisha kusitisha ushirikiano na IAEA kufuatia azimio la kisiasa
Jul 02, 2025 08:24Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, ameidhinisha rasmi sheria ya kusitisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) kufuatia azimio la kisiasa lililochochea hatua za uchokozi kutoka Marekani na Israel dhidi ya Iran.