-
Iran inachunguza ombi la Marekani kuhusu kuanza tena mazungumzo ya nyuklia
Jul 12, 2025 03:38Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amethibitisha kuwa Iran imepokea ombi kutoka Marekani kuhusu kuanza tena mazungumzo ya nyuklia, na amesema kwa sasa Tehran inachunguza pendekezo hilo kwa kina.
-
Iran yaijia juu Marekani kwa kumwekea vikwazo Ripota wa UN
Jul 11, 2025 12:36Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei ameikosoa vikali Marekani kwa kumwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Tuhuma dhidi ya Iran zaendelea licha ya Grossi kukiri tena kwamba Iran haitengenezi silaha za nyuklia
Jul 11, 2025 23:04Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesisitiza kuwa, hakuna ushahidi wa kuaminika kwamba Iran imepata silaha za nyuklia na kusisitiza ulazima wa kutatuliwa kidiplomasia suala la nyuklia la Iran.
-
Kamanda: Hatutaruhusu hata shibri moja ya ardhi ya Iran itwaliwe
Jul 11, 2025 11:52Mkuu wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesisitiza kuwa wanajeshi wa nchi hii hawataruhusu hata shubri moja ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu kuporwa.
-
Picha za satalaiti zamsuta Trump; Iran ilikiharibu vibaya sana kituo cha US Qatar
Jul 11, 2025 11:14Picha mpya za satelaiti zimefichua uharibifu mkubwa uliotokea katika kituo cha anga cha Marekani cha Al Udeid kilichoko nchini Qatar baada ya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanywa na Iran mwezi uliopita, na hivyo kusuta madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba kambi hiyo kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi haikudhurika.
-
Iran: Marekani lazima ifidie makosa yake kabla ya mazungumzo
Jul 11, 2025 04:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mheshimiwa Seyyed Abbas Araghchi, amesema kuwa Tehran iko wazi kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Marekani kwa msingi wa kuheshimiana pande zote.
-
Qalibaf: Waisraeli wasiopungua 500 waliangamizwa katika vita na Iran
Jul 10, 2025 23:41Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Qalibaf amesema kusitishwa kwa uvamizi wa kijeshi wa hivi karibuni wa Israel dhidi ya Iran kulitokana na kushindwa kwa utawala huo, na wala sio kutokana na kujizuia kwa upande wake.
-
Zarif aikosoa US kwa kumwekea vikwazo ripota wa UN
Jul 10, 2025 16:54Aliyekuwa Makamu wa Rais katika Masuala ya Kistratajia wa Iran, Mohammad-Javad Zarif amekosoa hatua ya Marekani ya kumuwekea vikwazo Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Rais wa Iran: Uchokozi wowote utakaorudiwa utakabiliwa na jibu kali zaidi na la kujutisha zaidi
Jul 10, 2025 11:33Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa, uchokozi wowote utakaorudiwa kufanywa dhidi ya ardhi ya Iran utakabiliwa na jibu kali zaidi na la kujutisha zaidi.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Tumejiweka tayari kujibu chokochoko zozote za Israel
Jul 10, 2025 10:14Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vimejipanga kikamilifu kutoa jibu kali kwa chokochoko zozote zitakazofanywa na utawala mtendaji jinai wa kizayuni wa Israel na waungaji mkono wake wa Magharibi.