Baghaei: Utawala wa Israel ulikiuka usitishaji vita Gaza tangu mwanzo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132754-baghaei_utawala_wa_israel_ulikiuka_usitishaji_vita_gaza_tangu_mwanzo
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa: "Tangu maelewano ya amani yalipoanzishwa na kuanzishwa usitishaji vita huko Gaza, badala ya dhana ya "kusitisha mapigano," tunakabiliwa na ukweli wa "ukiukaji wa usitishaji vita."
(last modified 2025-11-03T11:52:57+00:00 )
Nov 03, 2025 10:12 UTC
  • Baghaei: Utawala wa Israel ulikiuka usitishaji vita Gaza tangu mwanzo
    Baghaei: Utawala wa Israel ulikiuka usitishaji vita Gaza tangu mwanzo

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa: "Tangu maelewano ya amani yalipoanzishwa na kuanzishwa usitishaji vita huko Gaza, badala ya dhana ya "kusitisha mapigano," tunakabiliwa na ukweli wa "ukiukaji wa usitishaji vita."

Esmail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari leo, ambapo amezungumzia kuwadia Novemba 4, na kuitaja kuwa ni siku isiyoweza kufa katika kumbukumbu ya taifa la Iran na kuwa ni ishara ya muqawama, kuusimama kidete, kuhifadhi uhuru, na heshima ya kitaifa ya watu wetu wapendwa."

Jumanne ya kesho tarehe 4 Novemba 2021 inasadifiana na maadhimisho ya Aban 13 kwa kalenda ya Kiirani ambayo ni siku ya kupambana na ubeberu wa dunia humu nchini.

Itakumbukwa kuwa tarehe 13 Aban 1358 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 4 Novemba 1979, wanafunzi wa chuo kikuu wa Iran walilivamia pango la kijasusi la Marekani mjini Tehran lililokuwa na ubalozi wa dola hilo la kibeberu baada ya kuongezeka njama za Marekani za kutaka kufanya mapinduzi mengine nchini Iran.

Akizungumzia matukio ya eneo Baghaei amesema: "Bado tunashuhudia muendelezo wa mauaji ya halaiki na maangamizi makubwa ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Katika kipindi hiki kifupi, tangu kuibuliwa suala la usitishaji vita, zaidi ya Wapalestina 200 wasio na hatia wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni."