Tetemeko la ardhi laikumba Afghanistan, makumi waripotiwa kufariki dunia
-
Tetemeko la ardhi laikumba Afghanistan, makumi waripotiwa kufariki dunia
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 kwa vipimo vya richter limeikumba Afghanistan usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya makumi ya watu.
Taarifa za awali zinasema kuuwa, watu 20 wameaga dunia na mamia ya wengine kuujeruhiwa.
Hata hivyo mamlaka za Afghanistan zinasema kuwa, kuna uwezekano wa kuongezeka idadi ya vifo kutokana na baadhi ya watu kutoweka baada ya janga hilo la kimaumbile.
Shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga huko Afghanistan limesema litatoa taarifa kuhusiana na vifo au hasara zitatolewa baadae.
Shirika la kuchunguza matetemeko ya ardhi la Marekani la USGS limesema kuwa, lilipata tahadhari katika mfumo wake inayoonyesha kuwa kuna uwezekano wa wahanga wengi kutokana na tetemeko hilo na kwamba kuna uwezekano wa kuwa janga hilo limetokea katika maeneo mengine pia.
Tetemeko hilo limepiga kina cha kilomita 28 ardhini na karibu na Mazar-e Sharif, mji ulio na karibu watu 523,000.
Video za juhudi za kuwaokoa watu waliokuwa wamenasa chini ya vifusi zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Tetemeko hilo la ardhi nchini Afghanistan limetoa chini ya miezi miwili baada ya nchi hiyo kukumbwa na janga jingine kama hilo mwezi Septemba mwaka huu ambapo zaidi ya watu 800 waliaga dunia.
Tetemeko la ardhi la mwezi Septemba nchini Afghanistan lilipiga mkoa wa kaskazini-mashariki mwa Afghanistan wa Kunar.
Oktoba 2023, tetemeko la ardhi lilipiga mkoa wa Herat magharibi mwa Afghanistan, na kuua takriban watu 2,400 wka mujibu wa takwimu za serikali ya Kabul.