Umoja wa Afrika wampongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i132716-umoja_wa_afrika_wampongeza_samia_suluhu_hassan_kwa_kuchaguliwa_kuiongoza_tanzania
Umoja wa Afrika umempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuingoza Tanazania kwa muhula mwigine baada ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 mwezi uliopita wa Oktoba.
(last modified 2025-11-02T11:28:14+00:00 )
Nov 02, 2025 11:28 UTC
  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
    Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Umoja wa Afrika umempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuingoza Tanazania kwa muhula mwigine baada ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 29 mwezi uliopita wa Oktoba.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mahmoud Ali Youssouf amempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Youssouf ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu kupotea kwa maisha ya watu wakati wa maandamano ya baada ya uchaguzi na kutoa rambirambi kwa familia za waathiriwa.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) "amesisitiza umuhimu wa kutetea haki na uhuru wa msingi, ikiwa ni pamoja na haki ya kukusanyika na kujieleza kwa amani, na amehimiza mamlaka kulinda haki hizi ndani ya mfumo wa sheria."

Vilevile Youssouf ametoa wito kwa Watanzania kutekeleza haki zao kwa njia ya amani na uwajibikaji, na  kusisitiza tena kanuni za Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, pamoja na kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu, na uhuru kama msingi wa jamii za kidemokrasia na imara. 

Samia Suluhu Hassan anakuwa rais wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa nchini Tanzania. Awali alihudumu kama makamu wa rais kuanzia 2015 hadi 2021 na alichukua madaraka ya mchi kwa mara ya kwanza Machi 2021 kufuatia kifo cha Rais wa wakati huo, John Magufuli, ikiwa hatua muhimu ya kihistoria kama rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania.

Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, INEC, imtangaza Samia Suluhu Hassan mshindi wa uchaguzi huo wa rais. Samia Suluhu Hassan ameibuka mshindi kwa kupata 98 ya kura. 

Uchaguzi wa sasa wa Tanaania uliandamana na ghasia na machafuko ambayo baadhi ya duru zinasema yamepelekea kuuawa watu kadhaa.