Tanker Trackers: Iran imepakia mapipa milioni 4.6 ya mafuta ghafi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138000-tanker_trackers_iran_imepakia_mapipa_milioni_4.6_ya_mafuta_ghafi
Taasisi ya Ufuatiliaji wa Meli za Mafuta (Tanker Trackers) imetangaza kuwa Iran imepakia mapipa milioni 4.6 ya mafuta ghafi katika vituo vyake vya kuuza nje bidhaa hiyo.
(last modified 2026-04-27T12:47:52+00:00 )
Apr 27, 2026 12:09 UTC
  • Meli ya mafuta
    Meli ya mafuta

Taasisi ya Ufuatiliaji wa Meli za Mafuta (Tanker Trackers) imetangaza kuwa Iran imepakia mapipa milioni 4.6 ya mafuta ghafi katika vituo vyake vya kuuza nje bidhaa hiyo.

Hatua hii inaonyesha kuwa Iran inaendelea na shughuli zake za usafirishaji wa mafuta nje ya nchi kama kawaida, na meli za kijeshi za Marekani hazina uwezo wa kuzuia njia zinazotumiwa na Iran.

Wakati huo huo, Shirika la Habari la Associated Press Jumamosi lilitangaza kuwa zaidi ya mapipa milioni 10 ya mafuta ya Iran yameondoka katika Ghuba ya Uajemi tangu Marekani ilipoimarisha mzingiro wa baharini katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takwimu zilizotajwa hapo juu zimetokana na data za makampuni ya kufuatilia meli za mafuta, ambazo zinaonyesha kuwa shehena kadhaa za mafuta ya Iran zimeweza kuvuka eneo linalofuatiliwa na wanajeshi wa Marekani katika siku za karibuni.

Kwa mujibu wa Associated Press, meli kadhaa za mafuta zilizobeba mafuta ghafi ya Iran ziliondoka katika Ghuba ya Uajemi hivi karibuni, na zilikuwa na zaidi ya mapipa milioni 10.