Jeshi la Iran laonya litatoa jibu kali iwapo mzingiro haramu wa baharini wa Marekani utaendelea
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137986-jeshi_la_iran_laonya_litatoa_jibu_kali_iwapo_mzingiro_haramu_wa_baharini_wa_marekani_utaendelea
Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran imeonya kuwa kuendelea kwa “uharamia, mzingiro, na uhalifu wa baharini” unaofanywa na vikosi vya Marekani katika eneo, utakabiliwa na jibu kutoka kwa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-04-26T11:29:10+00:00 )
Apr 26, 2026 11:27 UTC
  • Jeshi la Iran laonya litatoa jibu kali iwapo mzingiro haramu wa baharini wa Marekani utaendelea

Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran imeonya kuwa kuendelea kwa “uharamia, mzingiro, na uhalifu wa baharini” unaofanywa na vikosi vya Marekani katika eneo, utakabiliwa na jibu kutoka kwa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kamandi ya Khatam al-Anbiya ya Jeshi la Iran imetoa taarifa na kusema kwamba:“Iwapo jeshi la Marekani litaendelea na mzingiro wake wa kihalifu, uharamia na uporaji wa baharini katika eneo hili, basi na wajue kwa yakini kuwa watakabiliwa na jibu la vikosi vyetu vyenye nguvu.”Kamandi hiyo imesisitiza kuwa jeshi la Iran hivi sasa lina “nguvu na utayari mkubwa zaidi” kuliko hapo awali katika kulinda mamlaka ya taifa, mipaka ya ardhi na bahari, pamoja na maslahi ya kitaifa.Aidha, kamandi hiyo imeikumbusha Washington kuwa baadhi ya vitengo vya jeshi la Marekani tayari vilishuhudia uwezo wa mashambulizi wa Iran wakati wa hujuma ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, iliyoanza tarehe 28 Februari.Taarifa hiyo pia imebaini azma ya Iran kuendelea kufuatilia kwa karibu mienendo ya adui katika eneo la Asia Magharibi, huku ikiendelea kudhibiti kikamilifu Mkondo wa kimkakati wa Lango Bahari la Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa nishati na biashara ya kimataifa.Katika sehemu nyingine taarifa hiyo imeongeza kuwa:“Tuko tayari na tuna azma thabiti ya kuwasababishia hasara kubwa zaidi wavamizi wa Kimarekani na Kizayuni iwapo kutatokea uvunjaji wowote mpya.”Mvutano umeongezeka kufuatia kile kinachotajwa kuwa ni mzingiro wa baharini unaotekelezwa na Marekani dhidi ya bandari na meli za Iran, pamoja na juhudi za Marekani za kuondoa mabomu ya baharini katika Lango Bahari la Hormuz.Maafisa wa Iran wamesema kuwa mzingiro huo ni kinyume cha sheria za kimataifa na ni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa tarehe 8 Aprili, na ambayo baadaye yaliongezwa kwa uamuzi wa upande mmoja na Rais wa Marekani, Donald Trump, saa chache kabla ya muda wake wa kuisha tarehe 22 Aprili.Iran imesisitiza kuwa haitakubali masharti ya kulazimishwa kutoka Marekani, na kwamba haitashiriki mazungumzo yoyote chini ya kivuli cha vitisho.