Mchambuzi wa siasa wa Marekani: Trump ndiye gaidi zaidi duniani
-
Donald Trump
Mchambuzi wa siasa wa Marekani, Kyle Kolinsky, amesema: Donald Trump, rais wa nchi hii, ndiye gaidi mkubwa zaidi duniani.
Kyle Kulinski amesema: "Wewe (Trump) ulilenga shule ya msingi ya Minab, nchini Iran, mara tatu. Umepiga mabomu hospitali, umeshambulia kwa makombora shule kadhaa, mitambo ya umeme na miundombinu ya raia nchini Iran. Wewe- anaendele kusema mchambuzi huyo wa siasa wa Marekani- ndiye mhalifu mkubwa wa kivita na gaidi wa magaidi wote wanaoua watu kwa njia ya kutisha."
Katika muktadha huu, wachuo na maprofesa katika Chuo Kikuu cha Berkeley nchini Marekani wameweka picha za wanafunzi waliouawa shahidi wa Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyibah ya Minab, nchini Iran, katika chuo hicho ili kuwakumbusha watu wa Marekani na wanasiasa kuhusu ukubwa wa janga hilo.
Zaidi ya wanafunzi 165 na walimu wao 27 waliuawa katika shambulizi la kigaidi la Marekani katika siku ya kwanza ya mashambulizi ya nchi hiyo ikishirikiana na utawala wa kikatili wa Israel dhidi ya Iran, tarehe 28 Februari mwaka huu.