Qalibaf ajibu madai ya Trump na Waziri wa Fedha wa US
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138078-qalibaf_ajibu_madai_ya_trump_na_waziri_wa_fedha_wa_us
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amejibu madai ya Rais wa Marekani na majigambo ya Waziri wa Fedha wa utawala huo wa kigaidi kupitia ujumbe uliotumwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.
(last modified 2026-04-30T10:25:17+00:00 )
Apr 30, 2026 10:21 UTC
  • Mohammad Baqer Qalibaf
    Mohammad Baqer Qalibaf

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amejibu madai ya Rais wa Marekani na majigambo ya Waziri wa Fedha wa utawala huo wa kigaidi kupitia ujumbe uliotumwa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.

Mohammad Baqer Qalibaf, amejibu madai ya uongo ya Donald Trump kuhusu kulipuka visima vya mafuta vya Iran kwa kuandika: "Siku tatu zimepita na hakuna visima vya mafuta vilivyolipuka."

Tunaweza kuongeza muda huo hadi siku 30 na kuonyesha picha za moja kwa moja za visima,” amesema Qalibaf.

Ameongeza kuwa: "Maelezo kama haya ni upuuzi ambao serikali ya Marekani inapokea kutoka kwa watu kama Scott Besant (Waziri wa Fedha wa nchi hiyo), ambao pia wanaeneza fikra ya kuendeleza mzingiro na kupandisha bei ya mafuta hadi zaidi ya dola 120."

Spika wa Bunge la Iran amesema hatua inayofuata bei ya mafuta itapanda na kufikia dola 140 kwa pipa.

Qalibaf amesisitiza kuwa: "Tatizo si mawazo potofu tu, bali pia jinsi ya kufikia na akili mbovu."