Uharamia wa Marekani utakabiliwa na majibu makali Iran ambayo hayajawahi kuonekana
Uharamia na ujangili wa baharini unaoendelezwa na Marekani utapata majibu ya Iran ambayo yatakuwa ya 'kivitendo na ya kipekee.
Chanzo cha juu cha usalama kimeiambia Press TV kwamba Majeshi ya Iran, chini ya kamandi ya vita ijulikanayo kama Makao Makuu ya Khatam al‑Anbiya , yanaamini kuwa uvumilivu una mipaka, na kwamba hatua kali inahitajika iwapo Marekani itaendelea na mzingiro wake wa kivita usio halali katika Lango Bahari la Hormuz.
Chanzo hicho kiliendelea kusisitiza kuwa Iran imeonyesha katika vita vilivyolazimishwa kwamba Marekani sasa inakabiliwa na mpinzani ambaye si tegemezi wala tabirika.
Kupitia uimara wa wananchi na majeshi yake, na chini ya uongozi wa hekima, ujasiri na maamuzi makini wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, Iran imefanikiwa kudhoofisha na kuondoa itibari ya chaguo zote za Marekani zilizo mezani.
Chanzo hicho kilifafanua kuwa uvumilivu ulioonyeshwa na majeshi ya Iran hadi sasa ulikusudiwa kutoa nafasi kwa diplomasia, ili Marekani iweze kufahamu na kukubali masharti ya Iran kwa ajili ya kumaliza vita kikamilifu.
Muda huo wa kujizuia ulikuwa fursa kwa Rais Donald Trump kuiondoa Marekani kwenye hali ngumu ya kisiasa na kijeshi iliyojiingiza nayo.
Hata hivyo, ikiwa ukaidi na dhana potofu za Marekani zitaendelea na masharti ya Iran yatakataliwa, afisa huyo alionya kuwa adui anapaswa kutarajia majibu tofauti kwa mzingiro wa baharini unaoendelea ambao kimsingi ni uharamia wa baharini.