Takriban watu 20 wanahofiwa kufariki dunia baada ya boti kuzama nchini Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138072-takriban_watu_20_wanahofiwa_kufariki_dunia_baada_ya_boti_kuzama_nchini_uganda
Ripoti kutoka Uganda zinasema kuwa shughuli za utafutaji na uokoaji zilikuwa zikiendelea magharibi mwa nchi hiyo siku ya Jumatano baada ya boti kupinduka kwenye mto Nguse nchini humo.
(last modified 2026-04-30T08:45:23+00:00 )
Apr 30, 2026 08:42 UTC
  • Watu 20 wanahofiwa kufariki dunia Uganda baada ya boti kuzama
    Watu 20 wanahofiwa kufariki dunia Uganda baada ya boti kuzama

Ripoti kutoka Uganda zinasema kuwa shughuli za utafutaji na uokoaji zilikuwa zikiendelea magharibi mwa nchi hiyo siku ya Jumatano baada ya boti kupinduka kwenye mto Nguse nchini humo.

Zaidi ya watu 30 walikuwa kwenye boti hiyo wakati ilipozama Jumanne jioni.

Watu wanane walionusurika katika ajali hiyo ya boti wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali. Mamlaka husika ya Uganda imewataka ndugu wa waathirika kujitokeza. 

Polisi wa majini katika wilaya ya Kigadi wameanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo. Wanasema sababu zinazowezekana ni pamoja na kupakia mzigo kupita kiasi, usafiri wa usiku na hali mbaya ya boti yenyewe.

Eneo la Kigadi limekumbwa na ajali nyingi za boti katika miaka ya hivi karibuni, hasa katika Ziwa Victoria upande wa Uganda

Vilevile mamia ya watu walipoteza maisha wakati feri ya abiria ilipozama upande wa Tanzania wa ziwa hilo mwaka 2018.