IRGC: Manowari za Marekani zitateketea ikiwa Iran itashambuliwa tena
-
Brigedia Jenerali Seyyed Majid Mousavi
Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Seyyed Majid Mousavi, amesema Iran itajibu uchokozi wowote wa adui kwa mashambulizi ya muda mrefu na yenye kuumiza, akibainisha kuwa meli za kivita za Marekani zitapata hatima sawa na vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi.
Katika onyo lake kwa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati (CENTCOM), Jenerali Mousavi alijibu taarifa za mipango ya Marekani kufanya “mfululizo wa mashambulizi mafupi lakini makali” yakilenga miundombinu ya Iran.
Ameandika katika ujumbe wake kwamba: “Mmeyaona yale yaliyotokea kwa vituo vyenu katika eneo. Hatima sawa na hiyo pia itazikumbe meli zenu za kivita.”
Onyo hilo linakuja wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kupokea taarifa maalumu Alhamisi kutoka kwa Kamanda wa CENTCOM, Admeri Brad Cooper, kuhusu mipango mipya ya uwezekano wa shambulio la kijeshi dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mawasilisho hayo yanaashiria kuwa Trump anafikiria kwa uzito kuhusu mashambulizi ya kijeshi ya kiwango kikubwa, ili kuvunja mkwamo katika mazungumzo au kutoa kile jarida la Axios ilidai kuwa ni “pigo la mwisho kabla ya kumaliza vita”.
Ripoti hiyo ilisema CENTCOM imeandaa mpango wa “mfululizo wa mashambulizi mafupi na makali” dhidi ya Iran, yanayoweza kulenga miundombinu muhimu.
Pendekezo jingine lisilo la kimantiki, linalotarajiwa pia kuwasilishwa, linahusiana na “kudhibiti sehemu ya Mlango wa Bahari wa Hormuz ili kuufungua upya kwa meli za kibiashara”, operesheni ambayo inaweza kujumuisha vikosi vya nchi kavi.
Axios, chombo hicho cha habari kinachounga mkono utawala wa Kizayuni imedokeza apia kuw. “Chaguo jingine lililowahi kujadiliwa, na huenda likafufuliwa tena, ni operesheni ya vikosi maalum kwa ajili ya kupora akiba ya Iran ya urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha juu,”
Axios ilinukuu Trump akisema Jumatano kuwa anaona mzingiro wa baharini dhidi ya Iran kuwa “wenye ufanisi zaidi kiasi kuliko mabomu”, ingawa bado yuko wazi kwa hatua za kijeshi ikiwa Iran haitasalimu amri.
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilifanya mashambulizi makali kwa muda wa siku 40, yakilenga mali za kijeshi za Marekani na Israeli katika eneo, baada ya pande hizo mbili kufanya hujuma za kigaidi dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa Iran pamoja na miundombinu ya kijeshi na kiraia.
Marekani ililazimika kutangaza upande mmoja kusimamisha mapigano kwa wiki mbili mnamo Aprili 8, ili kuruhusu mazungumzo kufanyika Islamabad. Hata hivyo, mazungumzo hayo yalivunjika baada ya Marekani kushindwa kupata kile ambacho haikuweza kukipata kwa njia ya mashambulizi ya kijeshi.