Kongo: Tumetungua droni ya jeshi la Rwanda
Jeshi la Kongo limetangaza kuwa limeidungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tukio hilo lililojiri katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia linaashiria kuongezeka mivutano kati ya nchi hizo mbili.
Ndege hiyo isiyo na rubani ilitunguliwa na jeshi la Kongo ikiwa katikati ya safari katika anga ya eneo la Point Zero katika Milima ya Minembwe huko Fizi.
"Kitendo hiki cha uhasama ni ukiukaji wa wazi wa anga ya nchi yetu, ni uchokozi wa wazi dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na jaribio jipya la kuvuruga utulivu katika eneo lililo chini ya uangalizi wa hali ya juu wa kioperesheni,” imesema taarifa iliyotiwa saini na kaimu msemaji wa jeshi Kongo, Luteni Kanali Mak Hazukay.
Hadi sasa Jeshi la Rwanda halijatoa taarifa yoyote kuhusu kutunguliwa droni yake katika anga ya Kongo.