-
Iran: UN isipendelee upande wowote, ikabiliane na ukiukwaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Marekani na Israel
Oct 27, 2025 08:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametaka Umoja wa Mataifa kuwakilisha kwa dhati haki za mataifa yote, huku akilaani uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran na msimamo wa kupendelea upande mmoja wa Baraza la Usalama la umoja huo.
-
Shirika la Kitaifa la Vipaji la Iran lawatunuku washindi 17 wa medali za Olimpiadi za Sayansi
Oct 27, 2025 08:44Shirika la Kitaifa la Vipaji la Iran (INEF) limeandaa hafla maalum ya kuwatunuku wanafunzi 17 wenye vipaji na vijana waliotwaa medali za dhahabu, fedha na shaba katika mashindano ya kimataifa ya Olimpiadi za Sayansi katika nyanja za Akili Mnemba (AI), Astronomia na Fizikia ya Anga, Uchumi, na Sayansi ya Kompyuta.
-
Velayati: Iran, Russia na China zina mchango madhubuti katika kuunda mfumo mpya wa dunia
Oct 27, 2025 08:43Mshauri mwandamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Dkt. Ali Akbar Velayati, amesema kuwa Iran, China na Russia, kama mataifa matatu huru yenye nguvu barani Asia, yana nafasi muhimu katika kuunda mfumo mpya wa dunia.
-
Iran: Hatua za mabavu zinazuia ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na uhalifu
Oct 27, 2025 03:15Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Vahid Jalalzadeh ambaye alielekea Vietnam kwa lengo la kuhudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Uhalifu wa Mtandaoni, amehutubia katika hafla hiyo na kusema: Mkataba wa Uhalifu wa Mtandaoni ni hatua muhimu kuelekea upande wa kuanzisha mfumo wa kimataifa wa kupambana na uhalifu wa mtandao na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
-
Kanali mstaafu wa jeshi la Marekani: Israel itaangamizwa ikiwa itaishambulia tena Iran
Oct 26, 2025 23:56Lawrence Wilkerson, kanali mstaafu wa jeshi la Marekani ametahadharisha kuhusu hatua yoyote ya Israel ya kuivuta Marekani katika vita na Iran na kusema kuwa Israel inaelewa vyema kwamba itaangamizwa ikiwa itaishambulia Iran bila ya kusaidiwa na upande wowote.
-
Qalibaf: Barua ya Iran-Russia-China kwa UN inaonesha mshikamano wa kimkakati dhidi ya vikwazo
Oct 26, 2025 08:31Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, barua ya pamoja ya hivi karibuni iliyotumwa na Iran, Russia na China kwa Umoja wa Mataifa kupinga jaribio la nchi za Ulaya la kurejesha vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu inaonesha "mshikamano wa kimkakati" uliopo baina ya mataifa hayo matatu yenye nguvu.
-
Araghchi: Iran iko tayari kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani kwa msingi wa kuheshimiana
Oct 26, 2025 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Tehran iko tayari kushiriki katika mazungumzo ya kidiplomasia na Marekani ili kufikia “suluhisho la busara” kuhusu suala la nyuklia, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana pande zote.
-
Iran: Lazima kuwe na kikomo cha kutoadhibiwa Utawala wa Kizayuni
Oct 25, 2025 09:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kwamba hali ya kutoadhibiwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, ambayo imepewa uhalali na wale wanaounga mkono utawala huo, inapaswa kukoma mara moja.
-
Iran: Baraza la Usalama halipaswi kukubali kudanganywa na kutumiwa vibaya
Oct 25, 2025 01:52Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema: Hati ya Umoja wa Mataifa imekumbana na mitihani mingi mizito kutokana na vitendo vya ukatili na kutumiwa vibaya kisiasa ya taasisi zake.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran: Trump ni mlea magaidi
Oct 24, 2025 06:41Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza kuwa Rais wa Marekani Donald Trump ni gaidi, na iwapo dunia inataka kumtambua gaidi halisi, basi mtu huyo si mwingine bali ni Trump mwenyewe.